• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI - MAJALIWA

Wakati ilipowekwa: October 1st, 2025

Asema Serikali kuwa lishe ni nguzo ya maendeleo ya rasilimali watu, uchumi na jamii

 Asema kiwango cha uzito uliozidi na uzito kupita kiasi hasa wanawake wa umri wa kuzaa kimeongezeka

WAZIRI MKUU, Mhe Kassim Majaliwa amesema kuwa kiwango cha udumavu miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano nchini kimeshuka kutoka asilimia 48 mwaka 1992 hadi asilimia 30 mwaka 2022.

Ameongeza kuwa, kiwango cha ukondefu miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano kimepungua kutoka asilimia 5 mwaka 1992 hadi asilimia 3.2 mwaka 2022.

Amesema hayo leo Jumanne (Septemba 30, 2025) wakati alipofunga mkutano wa 11 wa wadau wa lishe nchini, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa APC uliopo Bunju Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa lishe si suala la kiafya pekee, bali ni nguzo ya maendeleo ya rasilimali watu, uchumi na jamii. “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na chakula cha kutosha, afya njema na lishe bora”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameendelea kuwa kinara wa mapambano dhidi ya utapiamlo kwa kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele kwa kuimarisha bajeti, kuboresha mifumo ya ufuatiliaji na uhamasishaji wa afua za lishe kuanzia ngazi ya taifa hadi vijijini.

“Jitihada hizi zilimuwezesha kupata tuzo ya Global Goalkeeper kutoka Taasisi ya Gates Foundation, kutokana na mchango wake mkubwa katika kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu, hususan kwenye afya ya mama, mtoto na lishe”.

Katika hatua nyingine, mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kiwango cha uzito uliozidi na uzito kupita kiasi (kiribatumbo) hasa miongoni mwa wanawake wa umri wa kuzaa kimeongezeka kutoka asilimia 28 mwaka 2015 hadi asilimia 37 mwaka 2022. “Changamoto hii inaakisi mabadiliko ya ulaji na mtindo wa maisha ulioikumba sio tu Tanzania bali dunia nzima“.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Wizara na Taasisi zote za umma na binafsi kutenge rasilimali za kutosha kwa ajili ya afua za lishe na kuziweka katika mipango yao ya kila mwaka ili kuongeza uwajibikaji na uendelevu katika kutekeleza mipango iliyopangwa.

Pia Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Taasisi za Utafiti na Vyuo vya Elimu ya juu kuendeleza tafiti katika masuala ya lishe pamoja na kuhakikisha ripoti za tafiti hizo zinatumika kuboresha sera na mikakati nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu)Ridhiwan Kikwete amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa wadau wote walioanishwa katika Mpango Jumuishi wa masuala ya Lishe wanaendela kutekeleza majukumu yao. "Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa Wizara zote zinaingiza masuala ya lishe katika mipango ya kibajeti kila mwaka"

Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kukamilisha zoezi la utafiti wa gharama za utapiamlo ambao ulilenga kubainisha gharama na athari za utapiamlo katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi

"Matokeo ya utafiti huo yatatumika kama nyenzo muhimu ya uhamasishaji wa viongozi wa juu wa Serikali na watunga sera, kupitia majukwaa mbalimbali ili kuchangia hatua zaidi katika mapambano ya kutokomeza utapiamlo hasa kwa watoto"

www.ngaradc.go.tz

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MHE COL MATHIAS KAHABI DC NGARA ATEMBELEA UJENZI WA BARABARA YA KIVUKONI RUSUMO.

    October 02, 2025
  • VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI - MAJALIWA

    October 01, 2025
  • BONANZA LA WATUMISHI MAKAO MAKUU, WALIMU NA WANANCHI LAFANYIKA WILAYA YA NGARA

    September 27, 2025
  • CHAFANYIKA KIKAO KAZI CHA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA LISHE - 2025 WILAYANI NGARA

    September 26, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa