- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Viongozi wa serikali na wa wadini katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuwaelimisha na kuwapa taarifa wananchi ya namna watakavyonufaika na uwekezaji katika hifadhi tegefu ya Burigi, ili waweze kutumia fursa hiyo kukuza kipato chao.
Rai hiyo ilitolewa Septemba 08, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, alipokuwa akiongea na wafanyakazi pamoja na wananchi katika ukumbi wa Halmashauri wa wilaya ya Ngara, wakati wa ziara yake ya siku moja katika Wilaya hiyo.
“Kwa hiyo nitoe rai kwa viongozi katika mamlaka yenu; katika maeneo yenu ya utendaji, hakikisheni ujumbe huu unwafikia wananchi, ili waendelee kupata taarifa ya jambo hili, ili waweze kuona watashiriki vipi katika uchumi wa moja kwa moja katika uwekezaji unaokwenda kufanyika pale.” Alisema Brigedia Jenerali Gaguti.
Kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera haitakubalika baada ya miaka mitatu wana Ngara na mkoa wa Kagera wakabaki ni watazamaji tu wakati fursa zipo; na kuongeza kwamba serikali imetanga fedha za kuweka miundombinu; hivyo ni jukumu la viongozi kutoa elimu kwa wananchi, ili waweze kutumia fursa hiyo.
Aidha, amesema kwamba kuna tabia ya baadhi ya watu kufikira kwamba kuwekeza lazima awe na mtaji mkubwa sana, na kudai kwamba suala siyo mtaji kwani mtu anaweza kuwa na fedha nyimgi asiwekeze; kinachotakiwa hapa ni mawazo ya mtu mmoja mmoja au ya vikundi.
“Kwa hiyo, ni vema wakati serikali inaendelea na mchakato wa kuweka miundombi yake katika hifadhi tengefu, sisi kama wanakagera wilaya ya Ngara ikiwemo, tuanze kufikiria tutanufaikaje na uwekezaji huo mkubwa.” Alisema Brigedia Jenelali Gaguti.
Amesema amejirisha kwamba hifadhi hiyo tengefu ina hali ni nzuri sana, wanyama wengi na mazingira mazuri kukidhi azma ya serikali, na kuongeza kwamba kama wanakagera kuna fursa nyingi za kuwanufaisha wananchi.
Wananchi walioongea na mtadao wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara walimsifu mkuu huyo wa mkoa kwa kuwapa taarifa za kuwepo kwa fursa hiyo; huku wakiahidi kuwekeza katika hifadhi hiyo tengefu pindi itakapokuwa hifadhi ya taifa.
Aidha, wamesema wanachohitaji si mtaji tu, bali elimu na taarifa za kutosha, ili waweze kuwa na uelewa kutosha kujua wanatakiwa kufanya nini, na ukomo wa uwekezaji kwa mtu mmoja mmoja na wa kikundi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa