- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wa sekondari waliowakilisha Halmashauri ya Wilaya ya Ngara katika michezo ya UMISSETA kimkoa wameng’aa baada ya kushinda michezo yote na vijana zaidi 35 kati ya 120 walichaguliwa kuuwakilisha mkoa wa Kagera kitaifa.
Kaimu Afisaelimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Marton James, ameyasema hayo ofisini kwake Mei 28, 2018, baada ya kuwasili kutoka katika michezo hiyo, iliyofanyika katika Chuo cha Ualimu cha Katoke wilayani Muleba.
Ndugu Marton amesema kwamba michezo hiyo ilianza Mei 21 hadi 25, 2018, ambapo wanafunzi kutoka Ngara, walibuka wa kwanza katika mpira wa miguu, kwa kuwashinda Biharamulo bao moja kwa nunge.
“Tumekuwa wa kwanza pia katika mpira wa pete na wa wavu, mpira wa kikapu tulikuwa wa pili, ambapo Bukoba Manispaa waliibuka wa kwanza, mpira wa wavu tulikuwa wa pili, Muleba walikuwa wa kwanza; hatukufanya vizuri katika mchezo wa riadha baada ya kuibuka wa tano kwa pointi 15.” Alisema Ndugu Marton.
Amewataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria michezi, kwani michezo inajenga afya na ajira, na kwamba baadhi ya wazazi wanatabia ya kuwazuia watoto wao wao, kwenda katika kambi za michezo kama ile ya UMISSETA, iliyofanyika Chuo cha Ualimu wilayani Muleba.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa