- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
OR – TAMISEMI
Wanafunzi wanaoshiriki Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) wametakiwa kuzingatia nidhamu, sheria na miongozo ya mashindano hayo, ili kuendelea kuipa heshima sekta ya michezo nchini.
Maelekezo hayo yametolewa leo Mei 6, 2024 na Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumorasmi, , elimu maalum na michezo ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Ernest Hinju wakati akizungumza kwenye baraza la UMITASHUMTA Mjini Tabora.
Ameitaka mikoa yote iliyoleta wanafunzi kushiriki michezo mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaoshiriki mashindano hayo ni wanafunzi wa shule za msingi na wenye umri usiozidi miaka 14, huku akiwatahadharisha watakaobainika kuhusika kwenye udanganyifu kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa waalimu Wakuu Shule za Msingi Tanzania Mwalimu Rehema Ramole, amesema kuwa michezo ni furaha, upendo na ajira hivyo washiriki wanapaswa kufuata taratibu zilizowekwa, ili kushiriki michezo hiyo kwa furaha na amani.
“Michezo hii inaendeshwa kwa taratibu zote za kimashindano, ndio maana mmesikia suala la kuzingatia nidhamu, sharia na miongozo limesisitizwa kwa sababu huo ndio msingi mkuu ambao ukifuatwa utaleta tija michezoni” ameeleza Mwalimu Rehema.
Mashindano ya UMITASHUMTA 2024 yanaambatana na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuasisiwa kwake, na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 8/06/2024 na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim majaliwa kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
UMITASHUMTA & UMISETA mwaka 2024 inanaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, huku Mkoa wa Tabora ukiwa ni mwenyeji kwa mwaka wa tatu mfulululizo.
Kauli Mbiu ya Mashindano hayo mwaka huu ni “Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu, michezo na Sanaa, Hima Mtanzania shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024”
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa