- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA-KAGERA
Tarehe 22/11/2023. Mhe. Kanali Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara, amepokea Timu ya Watalaam wa Tanroads Taifa na Mkoa wakiongozwa na Ndg Julius Luhuro - Enviromental engineer wamefika ofisini kwa Mkuu wa wilaya kujitambulisha Kwa ajili ya kuanza zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi kuhusiana na Miradi ya kijamii itakayowanufaisha wananchi wanaoguswa na Mradi wa Ujenzi na uboreshaji wa Barabara ya Lusahunga - Rusumo yenye urefu wa km 92.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ameendelea kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa mradi huu mkubwa wa ujenzi wa Barabara urefu wa Kilomita 92
Pia Mkuu wa Wilaya amemshukuru Mhe. Ndaisaba George Ruhoro Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa kuisemea Barabara hii na hatimae Mkataba wa ujenzi upo kwenye utekelezaji.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa