- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanafunzi wa O-Level katika shule ya sekondari ya Muyenzi, wametakiwa kuwatumia wanafunzi wa A-Level, ili wawasaidia katika masomo yao, wafanye vizuri katika mithani ya ndani na ya taifa.
Akiongea na wanafunzi Aprili 12, 2019 wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Muyenzi Afisaelimu Idara ya Sekondari Ndugu Fikeni Ezekiel Senzighe amesema kuanzishwa kwa tahsusi za sanaa na sayansi ni neema kwani watoto watafanyavizuri ikiwa watawatumia dada zao.
“Shule nyingi zinazokuwa na kidato cha tano na cha sita wanafunzi wa vidato vya chini wanafanya vizuri; kwa hiyo tunatarajia kwamba katika masomo ya Arts shule hii itafanya vizuri zaidi kwani dada zao watawasaidia.” Alisema Ndugu Fikeni.
Amewaambia washereheka kwamba shule ya ya sekondari Muyenzi imeongeza tahsusi za masomo ya sayansi, abapo kwa kuanza itakuwa na tahsusi ya CBG Chemistry, Biology na Geography, kwa hiyo kidato cha tano wataoingia mwezi Julai 2019 watasoma masomo ya sayansi.
Akijibu itawezekanaje wakati shule hiyo ilikuwa na mchepua wa sanaa, Afisaelimu huyo amesema shule ina maabara za kutosha zilizosheheni vifaa vya sayansi vya kutoshereza mahitaji kwa wanafunzi watakaosoma tahsusi ya CBG.
“Kukua kwa shule hii kitahsusi ni chachu katika kufanya vizuri zaidi hapo baadae kwani watakuwa msaada mkubwa kwa wadogo zao; kwa hiyo, vijana wa O-Level watumieni dada zenu wa A-Level pale mtakapokwama katika masomo yenu, ili wawasaidie.” Ndugu Senzighe.
Aidha, amewashukuru wazazi na uongozi wa Kata ya Rulenge kwa kuanzisha utaratibu wa wanafunzi kupata uji shuleni akidai kwamba mtoto anapokuwa ameshiba anakuwa na utulivu wa fikirana na utayari wa kupokea kile anachojifunza.
“Nimefarijika kusikia kwamba wanafunzi walau wanapata uji mwanafunzi anapopata chakula cha mchana au angalau uji anapata nguvu ya kuweza kuendelea na masomo yake; na anakuwa na nguvu ya kuweza kujifunza zaidi, lakini pia kunakuwa na amani darasani.” Ndugu Senzighe.
Katika risala zilizosomwa nyingi zimeonyesha changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo, ambazo ni pamoja na upungufu wa madarasa, madawati, matundu ya vyoo, ukosefu wa umeme na upungufu wa walimu.
Amesema kwamba katika sekta ya elimu mapungufu yapo na yako katika mawanda waliyoyataja, serikali inayafahamu na inaweka utaratibu ambao utayamaliza hatua kwa hatua, hata hivyo wakati serikali inajipanga kutatua changamoto muendelee kusoma kwa bidii ili muweze kufanya vizuri katika mitihani yenu.
Shule ya sekondari ya Muyenzi ilifanya mahafali ya sita ambapo wanafunzi wapatao 64 wanatarajia kufanya mtihani wa kuihitimu kidato cha sita Mei 06, 2019, huku wakitakiwa kuendelea kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili waweze kupata kile kilichowaleta shuleni hapo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa