• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Ngara District Council
Ngara District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya wilaya ya Ngara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa Nyuki
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Mipango na Ufuatiliaji wa Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu
        • Elimu ya Msingi
        • Elimu ya sekondari
        • Kwa wanafunzi
          • Mitihani iliyopita
            • Kidato cha IV
      • Maji
        • Maji Mjini
        • Maji Vijijini
      • Kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi na zimamoto
      • Usafi na Mazingira
    • MSM
      • Huduma katika MSM
      • Muundo wa MSM
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za kisheria
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili ya Msingi
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Nyumba ya Picha

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI JIJINI DAR-ES-SALAAM

Wakati ilipowekwa: March 27th, 2023


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Maafisa Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa taarifa za jinsi serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha miaka miwili imefanya.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Machi 27, 2023

“Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, mnao wajibu wa kuhakikisha mnatoa taarifa za jinsi serikali ilivyotatua shida hizo za wananchi kwani kwa kutofanya hivyo wapo watu wengine wataendelea kufanya upotoshaji wakati sisi wanahabari tunajua kuwa huo ni upotoshaji.”” Alifafanua.

Alisema jukumu la kuisemea serikali ni moja ya sehemu ya mawasiliano ya nje ya serikali kwa hivyo wanapaswa kuzingatia.

Alisema sambamba na hilo, aliwataka wanahabari wote wa serikali na binafsi wahakikishe wananchi wanapata elimu na  taarifa sahihi kuhusu faida na umuhimu wa miradi na mipango au shughuli zinazotelekezwa na serikali ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa sahihi kwa urahisi  zaidi na kwa wakati.

Aidha aliwataka wazingatie suala la uhuru wa kupata na kutoa habari unaoendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, Taratibu na kanuni na wadau wote kila mmoja atimize wajibu wake.

Aliwataka kuimarisha matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuongeza upatikanaji wa habari kwenye maeneo yenu.“Kila mmoja kutoka mahali alipo, tunazo taasisi za mitandao ya kijamii ambazo zinafanya kazi pamoja na serikali, endeleeni kuwashirikisha katika kutoa taarifa za kazi na shughuli za serikali.” Alisisitiza.

Pia aliwataka kushiriki kikamilifu kuitangaza vema Tanzania ndani na nje ya nchi hususan sula la amani na utulivu, fursa za biashara na uwekezaji, historia ya nchi na kuweka msisitizo katika kufuata maadili na mila za nchi na kutangaza mali kale na vivutio

Aidha aliwataka kuweka mbele uzalendo, uadilifu, uhuru na maslahi ya nchi ili kulijenga taifa na aliwakumbusha kuongeza ubunifu wa kusukuma ajenda za serikali kwa umma.

Halikadhalika aliwataka kujiendeleza ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknlojia.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema Kikao hicho ambacho kimewaleta pamoja Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali kutoka Bara na Visiwani  ni muhimu kwa ustawi na mchango wa kada hii katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.

“Kikao hichi kitatumika pamoja na mambo mengine kutathimini mchango wetu katika kusukuma ajenda mbalimbali za serikali na namna ya kuboresha mchango huo.” Alifafanua Mhe. Nnauye.

Katika hatua nyingine TAGCO kimempa tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika kuimarisha sekta ya Habari, demokrasia, uwazi, uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa nchini.

Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya TAGCO, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema,  “Sisi maafisa Habari Serikalini, tumemwelewa, tunamwamini na tunamuunga mkono kwa dhati, Anaishi anayoyasema na anayatenda kwa ustadi mkubwa.” Alisema Mhe. Nape.

Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Mawasiliano ya Kimkakati Injini ya Maendeleo".

Kitengo Cha Mawasiliano Ngara-DC

Matangazo

  • RATIBA YA MKUU WA WILAYA YA NGARA MHE COL MATHIAS J KAHABI TAREHE 18/11/2024 MPAKA TAREHE 24/11/2024 November 18, 2024
  • TANGAZO LA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOOMBA KUWAFUATA WENZA WAO November 19, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA WILAYANI NGARA KWENYE TARAFA ZA MURUSAGAMBA NA RULENGE November 22, 2024
  • SEMINA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA WASIMAMIZI WA VITUO IMEFANYIKA TARAFA ZA KANAZI NA NYAMIAGA November 24, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA TATU 2024/2025 WAFANYIKA UKUMBI WA COMMUNITY CENTRE NGARA MJINI

    May 07, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA ABUBAKARI MWASSA AENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDEKEO WILAYA YA NGARA

    May 03, 2025
  • MHE HAJJAT FATMA MWASSA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYA YA NGARA

    May 02, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE HAJAT FATMA MWASSA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI ZAFANA KIMKOA WILAYA YA NGARA

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUTEMBELEA TEMBO NICKEL WILAYANI NGARA KAGERA
Video za ziada

Kurasa za haraka

  • Reports
  • Acts
  • Application form
  • Organization Structure
  • E-MREJESHO

Kurasa mashuhuri

  • PSM (Public Service Management)
  • PO-RALG
  • NECTA
  • NACTE
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kutuma,kupokea na kufuatilia malalamiko,mapendekezo,maulizo na pongeza(eMalalamiko)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo la Ngara

Wasiliana nasi

    Ngara District Council

    Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara

    Simu ya mezani: 0282226016

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa