- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu Mhe Kasim Majaliwa Asema lengo ni kutimiza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia za kuwaletea Watanzania maendeleo.
Mhe Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wafanye kazi kwa bidii, weledi, nidhamu, uadilifu na ubunifu ili kutimiza maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo Watanzania.
Amesema kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu, mipango na mikakati wanayoisimamia yanahitaji Juhudi ya kila Mtumishi na nidhamu katika kufanya kazi.
Ametoa wito huo leo Jumamosi Novemba 11, 2023 katika kikao na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.
“Nitoe wito kwa kila Mtumishi kuzingatia nidhamu ya kazi na maadili ya utumishi wa umma, Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza falsafa ya Kazi Iendelee. Kwa msingi huo watumishi wote wa umma mnao wajibu wa kufuata na kutekeleza falsafa hii. ”
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa