- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara leo
Leo tarehe 23/04/2024 limefanyika zoezi la upandaji miti katika shule ya Ngara High School mgeni rasmi akiwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Mhe Col Mathias Julius Kahabi ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
TFS imetoa miti 2500 katika shule hiyo ikiwa mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Mhe Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Mgeni rasmi katika zoezi ilo alikuwa ni Mhe Mkuu wa wilaya ya Ngara, Col Mathias Julius Kahabi ambae amewakilishwa na meneja bwana Mussa Mlenge kutoka TFS kwa kuzingatia Kauli mbiu ya miaka 60 ya muungano "tumeshikamana na tumeimarika, kwa maendeleo ya Taifa letu ". Amesisitiza uongozi wa shule kuendelea kutunza miti hiyo ambapo TFS itaendelea kuisaidia shule katika uhifadhi wa mazingira.
Mkuu wa shule ya Ngara High School ameushukuru uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara pamoja na uongozi wa TFS Kwa kuwaletea miti katika shule yao pia TFS wameahidi kuwaletea miti ya matunda.
Mkuu wa shule Ngara High School akiongea na wageni waliofika shuleni hapo pamoja na kutoa utambulisho.
Meneja TFS bwana Mussa Mlenge akiongea na hadhara baada ya kufika shuleni ngara high school.
Wanafunzi wa shule ya Ngara High School wakichukua miti kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yaliyoandaliwa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
viongozi pamoja na wanafunzi katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
Mkuu wa shule, meneja wa TFS, watumishi kutoka TFS, pamoja na wanafunzi
Mkuu wa shule akikabidhi taarifa ya shule kwa mwakilishi wa mgeni rasmi.
Meneja wa TFS akipanda mti kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Ngara.
mkuu wa shule Ngara high school akipanda mti.
mwanafunzi akipanda mti kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya muungano.
zoezi la kupanda miti likiendelea.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa