- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
1.0 UMUHIMU WA KILIMO:
PICHA/JINA
|
CHEO
|
MAWASILIANO
|
Ndugu Constantine E. Mudende
|
Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
|
+255 784 979 637
kilimo@ngaradc.go.tz
|
1.1 Idara ya kilimo.
Idara ya kilimo inalenga kuleta huduma ya ushauri wa kitalaamu karibu na wakulima. Lengo kubwa likiwa ni kupunguza umasikini uliokithiri kwa kutumia njia kuu nne za uzalishaji ambazo ni ardhi, watu, mtaji na ujasiliamali. Asilimia 90 ya wakazi wa Ngara wanategemea kililmo ili kuendesha maisha yao ya kila siku. Matumizi ya ardhi Wilayani Ngara yapo kama ifuatavyo:-
1.2 KILIMO.
Kahawa ni zao la biashara ambalo linalimwa katika kata 19 kati ya kata 22 zilizopo hapa Wilayani Ngara ingawaje haizalishwi kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na Wilaya jirani za Karagwe na Muleba. Kiasi kinachozalishwa kwa mwaka ni kati ya tani 303 hadi 960 za kahawa safi. Mazao makuu ya chakula hapa Wilayani ni ndizi, maharage, muhogo na mazao mengine ya mizizi. Jitihada za kuongeza uzalishaji wa mazao haya unafanyika kupitia mashamba darasa ambapo wakulima hufundishwa mbinu bora za kilimo cha mazao hayo na baadaye wao kwenda kuzitumia katika mashamba yao.
Wilaya ina misimu 3 ya mazao ambayo ni vuli, masika na kipindi cha kiangazi ambapo wakulima hufanya umwagiliaji wa asili. Hali hizi za hewa huwezesha wakulima kuweza kuzalisha mazao mwaka mzima.
Upatikanaji wa mvua ni kiasi cha mm 800- mm1400 kwa mwaka.
2016/2017, Wilaya imelenga kulima hekta 64,940 za mazao mbalimbali ambazo zinatarajiwa kuzalisha tani 437,263.
1.6. HALI YA UMWAGILIAJI.
Wilaya inalo eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji hekta 5000. Kwa sasa hekta 3,200 zinalimwa kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji wa asili katika mabonde yote yaliyopo hapa Wilayani Ngara. Mabonde yaliyo mengi yana vijito vinavyotiririsha maji mwaka mzima kiasi cha kuwezesha Wilaya kutumia mabonde yake katika kilimo endelevu, Wilaya inategemea kuboresha kilimo cha mabondeni kwa kukamilisha ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Bigombo-Rulenge yenye ukubwa wa hekta 110 ambao ujenzi wake ulianzishwa na mradi wa DASIP. Zaidi ya kaya 762 zitanufaika na skimu hiyo. Yapo mabonde mengi ambayo yanaweza kutumika kwa shughuli za umwagiliaji ambayo ni, Mugozi (Hekta 540), Muhongo (Hekta 170), Nyarulama (Hekta 110), Ntobeye (Hekta580), Magamba (120Ha), Rwinyana (160Ha),Mpanyura (430), Mubuhenge (Hekta 94), Nzaza (Hekta 150), Murutabo (Hekata 100), Mukafigiri (Hekta 60), Kumwendo (Hekata 300) na Ngundusi (Hekta 110).
Uwepo wama eneo haya muhimu unawezesha kuanzisha ujenzi wa skimu za umwagiliaji ambazo zinaweza kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na mboga.
1.7SEKTA YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Wilaya ya Ngara inacho chama kimoja cha Ushirika wa wakulima kinachojishughulisha na uuzaji wa mazao hasa zao la kahawa ambalo ndilo zao kuu la biashara.
1.7.1 Hali ya maendeleo ya Vyama vya ushirika.
3.0 FOMU ZINAZOJAZWA NA WATAALAMU KWA AJILI YA SHUGHULI MBALIMBALI
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa