- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
SEKTA YA MIUNDO MBINU.
PICHA/JINA
|
CHEO
|
MAWASILIANO
|
Ndugu,
|
Kaimu Mhandisi Ujenzi (W)
|
+255 757 344 761
ujenzi@ngaradc.go.tz
|
Pia Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kupitia Idara ya Ujenzi inashughulikia kazi zote za Ujenzi wa Majengo mbalimbali katika idara tofauti kadri inavyohitajika pia idara inahudumia Mtandao wa Barabara zenye jumla ya urefu wa Kilomita 632.85 ambazo zimegawanyika katika makundi matatu
1. Barabara muungo (Collector roads) Km 166
2. Barabara mjazio (Fedeer roads) Km 443.9
3. Barabara za Mjini (Urban roads) Km 22.95
8.1 Hali ya barabara Wilayani.
Hali ya barabara ni nzuri kwa barabara zote za Wilaya , vijiji na mjini zinapitika vizuri kwa mwaka mzima.
8.2 Huduma za usafiri wa anga:
Wilaya inacho kiwanja kimoja (1) cha ndege kinachomilikiwa na Serikali chenye urefu wa km 1.7. Kipo Ruganzo km 10 toka Ngara Mjini upande wa kusini mashariki.
8.3 Umeme:
Wilaya inatumia umeme unaotokana na mitambo inayoendeshwa na nishati ya mafuta. Mashine hizo zina uwezo wa kutoa umeme kiasi cha megawati moja (1). Mwaka 2005 tulikuwa tunahudumia wananchi wa Ngara mjini pekee, hadi kufika mwaka 2015 tumeongeza idadi ya huduma ya umeme kwa wananchi wa mji mdogo wa Kabanga, Rusumo, Rulenge na Mugoma na vilevile kuendelea na mipango ya kusambaza umeme vijijini, Pia shirika la TANESCO linatarajia kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa megawati 80 katika maporomoko ya Rusumo.
8.4 Huduma za Simu:
Wilaya ya Ngara mwaka 2005 ilikuwa inapata huduma za simu katika mitandao ya CELTEL na TTCL, kufikia mwaka 2015 Wilaya inapata huduma nzuri ya simu kupitia Kampuni za VODA, AIRTEL,TIGO, NA TTCL.Lengo la Halmashauri kwa mwaka 2015 ni kuendelea na ushawishi kwa makampuni ya simu kupanua wigo wa mitandao yake.
8.5 Huduma za Posta:
Pia Wilaya inayo posta kamili ya Ngara Mjini yenye masanduku 500 na posta ndogo iliyoko Rulenge yenye masanduku 100. Kupitia posta yetu ya Ngara Mjini wilaya inapata huduma za mawasiliano ya kawaida pamoja na huduma za mawasiliano ya haraka (EMS) kwa barua na vifurushi. Pia wilaya imeingia kwenye mkongo wa Taifa ambao unarahisisha mawasiliano na hata kuwezesha mtandao wa mawasiliano hasa Internet kufanyakazi vizuri zaidi.
8.6 Huduma za Redio:
Wilaya inacho kituo cha redio kinachomilikiwa na Kanisa katoliki kinachojulikana kama “Redio kwizera FM”. Kituo hiki hurusha matangazo yake kuanzia Ngara, katika wilaya za Biharamulo, Kibondo, Kakonko, Kasulo na Sehemu ya wilaya chato na Karagwe.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa