- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HUDUMA YA UVUVI
Hakuna shughuli kubwa ya uvuvi inayofanyika, ingawa kuna mito mikubwa miwili iitwayo Kagera na Ruvuvu. , Uvuvi mdogo hufanyika kama njia ya kujikimu kimaisha. Samaki wa aina ya Tilapia (Oreochromis niloticus) na Kambale (Clarius gariepinus) wanafugwa katika mabwawa madogo ya ukubwa wa mita za mraba 200. Kuna mabwawa ya Samaki 59 ya kuchimba yanayoendeshwa na wakulima binafsi ama Vikundi vinavyowezeshwa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kama TCRS, TUMAINI FUND, and REDESO.
Halmashauri ya Ngara imeweka mpango wa kufufua Mabawa kwa kuyapanua na kujenga mapya ili kupata idadi kubwa ya samaki na kuongeza kipato.
Fursa za Sekta ya Uvuvi
Sekta ya Uvuvi inatoa fursa za uwekezaji ili kuongeza usalama wa chakula kwa kaya na pato la Taifa kwa Ujumla . Fursa hizo zipo katika maeneo yafuatayo:
(1) Uwekezaji katika Mbwawa ya samaki madogo na makubwa.
(2) Uvuvi katika mito ya asili.
(3) Uzalishaji wa mbegu bora ya samaki na chakula cha samaki..
(4) Utengenezaji wa vyombo na vifaa vya uvuvi na mahitaji mengine katika Sekta ya Uvuvi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa