- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
SEKTA YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA.
Bw. Enock Mponzi
|
CHEO
|
MAWASILIANO
|
|
Afisa Ardhi na Maliasili (W) | +255784501654
ardhi@ngaradc.go.tz
|
7.1 Misitu.
Wilaya ya Ngara inakadiriwa kuwa na eneo la misitu lipatalo hekta 105,000 . Misitu ya asili inachukua eneo lipatalo hekta 100,600 na misitu ya kupandwa ni hekta 4,400. Matumizi makubwa ya misitu hii ni kwa ajili ya matumizi ya kuni, nguzo za ujenzi na mbao.
Maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ni kama ifuatavyo:-
1. Msitu wa hifadhi Goyagoya hekta 1,434.
2. Pori la akiba Burigi (Upande wa Ngara ) hekta 13,500.
3. Pori la akiba Kimisi (Upande wa Ngara ) hekta 37,000.
7.2 Wanyamapori.
Sehemu ya mapori ya akiba ya Kimisi na Burigi iliyopo ndani ya wilaya ya Ngara inao wanyama jamii ya swala, tembo, nyati, twiga na viboko hupatikana katika mapori hayo. Mapori haya ya akiba yanaweza kuwa kivutio kikubwa kwa watalii endapo miundo mbinu itaboreshwa. Je mamba wapo ngara
6.3 Ufugaji Nyuki.
Kutokana na kuwepo misitu mingi na uoto wa asili shughuli za ufugaji nyuki hufanyika katika baadhi ya maeneo ya wilaya hii. Wilaya inakadiriwa kuwa na mizinga ya kisasa ipatayo 300 na mizinga ya kienyeji ipatayo 800. Maeneo yanayoongoza kwa ufugaji nyuki katika wilaya ya Ngara ni pamoja na kata za Nyakisasa, Rulenge, Rusumo, Kirushya, Bugarama na Murusagamba.
7.4 Utalii.
Wilaya inavyo vivutio kadhaa vya utalii ambavyo vikiendelezwa vinaweza kuongeza pato na kukuza uchumi wa wilaya. Vivutio muhimu ni kama ifuatavyo:-
1. Maporomoko ya Rusumo.
2. Mafiga matatu (Kasange)
3. Nyumba ya Mtemi-Kanazi
4. Mlima Shyunga (Mita 2,100 toka usawa wa bahari)
Wilaya imeisha ainisha maeneo haya imeishatafuta wadau mbalimbali kwa ajili ya kuyatangaza na kuyaendeleza. Mdau aliyeonyesha nia ya kuendeleza mpaka sasa ni KAYODEA.
7.5 Ardhi.
Kulingana na tangazo la serikali G.N No 176 la 1996 Sekta ya ardhi inaitambua miji ifuatayo kama maeneo yaliyoiva kuendelezwa kimji maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-
Ngara mjini, Kabanga, Rulenge, Kasulo, Rusumo, Murusagamba, Mugoma, Djuruligwa na Kanazi. Miji hii ina viwanja vilivyopangwa kwa matumizi mbalimbali kama iuatavyo:-
1. Viwanja vilivyopimwa 1,850
2. Viwanja vilivyogawiwa 1,670
3. Michoro ya mipango miji 12
4. Wastani wa makusanyo ya kodi za ardhi ni Tshs. Milioni 8.0 kwa mwaka.
Wilaya ina jumla ya mashamba 13 yenye ukubwa wa hekta 4,500. Pia ziko taasisi za Usimamizi wa maendeleo ya ardhi na Mazingira katika ngazi mbalimbali kulingana na miongozo ya kisekta kama ifuatavyo.
1. Mabaraza ya ardhi ya vijiji 68.
2. Kamati za mazingira za vijiji 50.
Mipango ya matumizi bora ya ard
ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO MAKAZI WILAYA YA NGARA MHE WILLIAM LUKUVI TAREHE 22.pdf
Idara ya Ardhi na Maliasili 2018.pdf
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa