- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI
PICHA/JINA
|
|
CHEO
|
|
MAWASILIANO
|
Bi. Jusline Bandiko
|
|
Afisa Elimu Msingi (W)
|
|
elimumsingi@ngaradc.go.tz
|
Katika Halmashauri ya Wilaya Ngara Idara ya Elimu Msingi ina jukumu la kusimamia na kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata Elimu iliyo bora katika maeneo yafuatayo; Elimu ya awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya watu wazima na Elimu ya ufundi Stadi.
IDADI YA SHULE, WANAFUNZI, ASASI MBALIMBALI NA UWIANO WA MWALIMU KWA WANAFUNZI
Tuna jumla ya Shule za Msingi 120 kati ya hizi 115 ni za Serikali na 5 si za Serikali. Katika shule hizi za Msingi pia kuna madarasa ya Awali 120 . Jumla ya Vituo vya MEMKWA ni 15 na Vituo vya Ufundi Stadi ni 5.
Jumla ya Wanafunzi wa Awali hadi Darasa la Saba kwa takwimu za Januari, 2016 ni 75,341 ( Wavulana 37,614; Wasichana 37,727) katika Shule za Serikali. Uwiano wa Mwalimu kwa Wanafunzi ni 1:46. Katika shule zisizo za serikali kuna jumla ya wanafunzi 899 (Wavulana 460; Wasichana 439). Hivyo jumla ya Wanafunzi wote ni 76,240 (Wavulana 38,074; Wasichana 38,166).
Kutokana na mwitiko mzuri wa jamii katika uandikishaji wa wanafunzi kwenye madarasa ya Awali na I, ifikapo tarehe 31 Machi, 2017 tutakuwa na ongezeko zaidi la wanafunzi. Hii ni kutokana na Mpango wa Serikali wa Elimu bila Malipo.
HALI YA MIUNDOMBINU : MADAWATI, VYUMBA VYA MADARASA, NYUMBA ZA WALIMU NA VYOO
Kwa mwaka 2016 Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imefanikiwa kuondoa tatizo la madawati kwa 100% hivyo wanafunzi wote kukaa kwenye madawati. Uhitaji mwingine wa madawati utatokana na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa Awali na Darasa la Kwanza kwa mwaka 2017. Kwa upande wa miundombinu mingine jitihada zinaendelea kuuondoa upungufu uliopo ambapo tayari mafanikio makubwa yamejitokeza. Mathalani, vyumba vya madarasa vya kudumu vilivyopo ni 46%, nyumba za walimu 16% na Vyoo 36%.
UTEKELEZAJI WA MTAALA NA MAENDELEO KITAALUMA KWA UJUMLA
Kwa jumla wananchi na wadau mbalimbali wa elimu: wanafunzi,walimu , wazazi, jamii, serikali na mashirika wamekuwa na ushirikiano mzuri – kila mmoja kwa nafasi yake hivyo kupelekea mazingira wezeshi na rafiki ya ujifunzaji na ufundishaji. Ushirikiano huu umeifanya Wilaya ya Ngara kufanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka katika mitihani ya kitaifa. Mathalani katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2016 ufaulu wa wanafunzi ulikuwa 87.82% kutoka asilimia 83.05 mwaka 2015; kuwa wa kwanza katika Mkoa wa Kagera kati ya Halmashauri 8, aidha kuwa wa 12 kitaifa kati ya Halmashauri 185.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa