- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
IDARA USAFI NA MAZINGIRA.
PICHA/JINA
|
CHEO
|
MAWASILANO
|
Ndugu, Zawadi Nicolaus Waziri
|
Kaimu Afisa Mazingira na Usafi
|
+255 684 998 788,/ +255 764 795 964
mazingira@ngaradc.go.tz
|
Idara ya usafishaji na mazingira ni moja ya Idara mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara iliyoanzishwa mwaka 2011 ikiwa inashughulikia mambo makuu yafuatayo:-
I. Kusimamia na kuratibu masuala yote yahusuyo usafi wa mazingira Wilayani,
II. Kusimamia na kuratibu masuala yote ya utunzaji wa mazingira, afya za binadamu, wanyama na mimea Wilayani,
III. Kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 kwenye Wilaya,
IV. Kushauri kamati ya usimamizi wa mazingira ya Wilaya kuhusu masuala yote ya mazingira,
V. Kukuza weledi kuhusu ulinzi wa mazingira na uhifadhi maliasili kwenye Wilaya,
VI. Kukusanya na kusimamia taarifa kuhusu mazingira na matumizi ya maliasili kwenye Wilaya,
VII. Kuandaa taarifa za mihula kuhusu hali ya mazingira ndani ya wilaya,
VIII. Kufuatilia maandalizi, mapitio na vibali vya tathmini ya Athari kwa mzingira kwa ajili ya uwekezaji wa ndani,
IX. Kufanya mapitio ya sheria ndogo zinazohusu usimamizi wa mazingira na shughuli maalumu za kisekta zinazohusiana na mazingira.
12.1 Vipaumbele vya Idara
I. Kuhimiza , kusimamia na kuendeleza usafi wa mazingira na jamii katika Wilaya
II. Kuhimiza na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za mazingira katika wilaya
III. Kupitia na kuendesha uchujaji wa miradi (Environment and social screening) kwa miradi yote inayotekelezwa ndani ya wilaya yetu ili kupunguza madhara ya kimazingira na kijamii.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa