- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara ni Wilaya moja kati ya wilaya nane zilizopo katika mkoa wa Kagera Magharibi mwa Tanzania bara. Umbali wa kutoka Ngara hadi Dare s Salaam ni km 1600 na makao makuu ya mkoa ni km 350. Wilaya ina pakana na nchi za Rwanda na Burundi. Wananchi wake wanaoishi mipakani huweza kuvuka mipaka, ili kutafuta huduma mbalimbali ikiwemo huduma za afya kutafuta ajira katika mradi mkubwa wa kutengeneza umeme wamaji uliopo katika maporomoko ya rusumo katika eneo hili kuna mkusanyiko mkubwa wa watu kutoka china,Rwanda,Burundi,Ethiopia,afrika ya kusini pamoja na watanzania kutoka mikoa mbalimbali nchini . kwa sasa hali hii inachangia kuenea kwa magonjwa mbalimbali ya zinaa na ukimwi katika eneo hili ambalo kimkoa wilaya ya Ngara ndiyo yenye maambukizi yaliyo chini kuliko wilayazote.hivyo mikakati ya kudhibiti maambukizi katika mkusanyiko huu isipowekwa mapema maambukizi yataongezeka kutoka asilimia 0.7 na kuendelea
HUDUMA ZA AFYA
Ngara ina vituo 61 vinavyotoa huduma za afya kati ya hizo 3 ni hospitali 5 ni vituo vya afya,na 53 ni zahanati. Vituo hivi vinahudumia watu 379050.
MAWASILIANO NA USAFIRI
Kuna barabara ya Rami kutoka isaka inaunganisha wilaya ya Ngara hadi Kigali Rwanda, Bujumbura Burundi na Dar e s salaam pia kuna bara za udongo zinazo unganisha mitaa na vijiji mbalimbali na pia kuna uwanja wa ndege wa Ruganzo umbali wa km 8 kutoka Ngara mjini.
MIPAKA ILIYOPO NGARA
Wilaya ya Ngara ime zungukwa na mipaka mitatu upande wa magharibi ni mpaka wa mursagamba upande mashariki ya kati kuna mpaka wa kabanga hii mipaka yote inaunganisha wilaya na Burundi. Pia kuna mpaka wa Rusumo unaounganisha na Rwanda vile vile kuna mipaka isiyorasmi kama vile mugoma ambayo pia inaunganisha na Burundi.
MAEGESHO YA MAGARI
Kando kando ya barabara kuu iendayo Kigali (RWANDA) Kuna maeneo ya kuegesha magari yaliyo tengwa kama ifuatavyo.
1.Muzani eneo la Murusagamba kuelekea mpakani Burundi
2.Benaco bara bara inayoelekea Rusumo kuelekea Rwanda
3.Ngara mjini barabara kuelekea Burundi kupitia Kabanga mpakani.
Sekta ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile shirika la MDH (Management and development for health) ICAP imeendelea kutekeleza mikakati ya Wizara ya Afya katika kukabiliana na ongezeko la maambukizi mapya ya VVU, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kutokomeza vifo vinavyotokana na VVU, kuondoa unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU, na kutokuwa na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI ifikikapo 2020. Na kwa awamu hii kuna mkakati 90,90,90. (Tisini ya kwanza ni asilimia ya wananchi wanaoishi na maambukizi wote wawe wamepimwa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI,na kujua hali zao .Tisini ya pili ya wale waliogundulika na maambukizi ya VVU baadayakupimwa wawe wameanzishiwa dawa, tisini ya tatu wale walio kwenye dawa wawe na ufuasi mzuri wa dawa na kiwango cha maambukizi) (viral load) kiwe chini sana.
MAFANIKIO
CHANGAMOTO
MIKAKATI
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa