- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
PICHA/JINA
|
|
CHEO
|
|
MAWASILIANO
|
Dr.Deogratius Mlandali
|
|
District Medical Officer
|
|
+255 625 606 758
afya@ngaradc.go.tz
|
Idara ya Afya imeendelea kutoa huduma za Afya kwa wananchi kupitia vituo vya huduma 61 ambavyo ni Hospitali 3 Vituo vya Afya 5 na Zahanati 53. Kati ya hivyo vituo vinavyo milikiwa na serikali ni hospital 1, Vituo vya afya 4 na zahanati 45. Huduma zimeendelea kutolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama MDH, SAPO, MARIA STOPES, JHPIEGO USAID-B0RESHA AFYA, Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kagera, Kanisa la katoliki Dayosisi ya Rulenge Ngara, PSI na Shirika la ABT ASSOCIATES.
UTEKELEZAJI WA HUDUMA ZA AFYA
UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA
Dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya zinapatikana kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na Bajeti kubwa inayotengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa, ikiwa ni pamoja na asilimia 67% itokanayo na makusanyo ya fedha za vituo vya huduma ambayo hutumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa.
HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO
Huduma hizi zimeendelea kutolewa katika vituo 54 kati ya vituo 61 kila siku ya kazi.
Utoaji wa huduma za chanjo na upimaji wa afya za watoto na akina mama wajawazito zimeendelea kutolewa kwa wananchi wanaoishi mbali na vituo katika maeneo 22 huduma ambazo hujulikana kama huduma za nje au (Mobile clinics) na huduma za mkoba 60 (Outreach Services). Kiwango cha uchanjaji kwa watoto wachanga na mama wajawazito kinaendelea vizuri kwa asilimia 94%. Idadi ya akina mama wanaojifungulia vituoni inaendelea kuongezeka hadi sasa asilimia 89%. wamejifungulia vituoni. Wahudumu wa afya wa vijiji ngazi ya jamii wanaendelea kutoa huduma ya kuelimisha jamii juu ya kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa rufaa pale wanapobaini kuwepo matatizo makubwa ya kiafya. Lengo la kufanya hivyo ni kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA
Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria yanaendelea. Ugunduzi wa ugonjwa wa malaria kwa kutumia vitendanishi ambavyo vinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya umefanyika. Dawa za tiba ya malaria zinapatikana katika vituo vya huduma kwa kiwango cha kuridhisha kwa zaidi ya 80%. Vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu vimegawiwa kwa wananchi kupitia shuleni. Wananchi wanaelimishwa umuhimu wa kupima kabla ya kutumia dawa kwani kipimo cha haraka cha kupima malaria kinapatikana katika vituo vyote. Wilaya ili endesha zoezi la unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani ili kuua mbu wa pevu waenezao ugonjwa wa malaria.
MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.
Mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI, vitendanishi vinaendelea kupatikana na kiwango cha maambukizi ni 0.7%.Wilaya imefanikiwa kupunguza kasi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kutokana na njitihada mbalimbali kama Upimaji wa hiari katika vituo vyote vya huduma za afya, Elimu ya kuzuia maambukizi katika mikutano mbalimbali ya jamii, Matumizi ya kinga kwa ajili ya kuzuia maambukizi kama vile mipira ya kiume na kike katika maeneo mbalimbali, Kuzuia maambukizi toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mototo kwa kuwahimiza akina mama kwenda na wenza wao waendapo kliniki ya ujauzito.Wilaya imefanikiwa kuanzisha vituo 9 kwa ajili ya tiba ya kufubaza Virusi vya UKIMWI. Na dawa zinapatikana katika vituo hivyo mapambano hayo pia yamefanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya Halmashauri na Wadau waliopo Wilayani hasa Shirika la “Management Development for Health
(MDH)”.
UPATIKANAJI WA RASILIMALI WATU
Idara ya afya inajumla ya watumishi 312 waliogawanyika katika kada mbalimbali kama ifuatavyo:-Daktari 6,madaktari wasaidizi 11,Afisa wauguzi 2,Afisa wauguzi wasaidizi 43,wauguzi 107,tabibu 27 tabibu wasaidizi 5,katibu wa afya 2,afisa afya mazingira 1,afisa afya mazingira msaidizi 6,wafamasia 2,wateknolojia dawa 4,wateknolojia maabara 4,wateknolojia wasaidizi maabara 12,wateknolojia wasaidizi dawa 1 na watumishi wengine 73 ambao ni wahudumu wa afya n wasaidizi wa afya mazingira. Kulingana na ikama watumishi waliopo ni asilimia 40.8%.na upungufu wa watumishi ni kwa asilimia 59.2%.
MAFANIKIO
Kuwepo Kwa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara katika vituo vyote vya huduma.
Kiwango cha chanjo kimeongezeka hadi asilimia 94%
Upimaji wa VVU umeendelea kufanyika katika vituo vya huduma na kiwango cha maambukizi asilimia 0.7%
Idadi ya akina mama wanaojifungulia vituoni ni asilimia 89%.
Vipimo kwa ajili ya ugunduzi wa vimelea vya Ugonjwa wa malaria vinapatikana katika vituo vya huduma.
Ukarabati wa vituo vya Afya viwili Mabawe pamoja na Murusagamba.
Idara imepokea watumishi 33wapya wa kada mbalimbali za afya
CHANGAMOTO
Bado kuna upungufu wa watumishi katika vituo vya huduma kwa asilimia 59.2%. Tatizo hili limeongezeka kutokana na watumishi kuhama kwa kasi.
Ucheleweshaji wa fedha toka vyanzo mbali mbali
Ongezeko la vifo vya wazazi kulinganisha na miaka ya nyuma mwaka 2017 vilikuwa 7, mwaka huu Januari hadi Juni vimefika vifo 12, sababu kuu zikiwa ni uambukizo, kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua. Akina mama kutowahi kwenye vituo vya huduma kwa ajili ya kujifungua.
Ongezeko la wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kisukari na magonjwa ya moyo.
MIKAKATI
Kuendelea kuomba vibali vya ajira toka Serikali
Kutoruhusu watumishi wengi kuhama kwa kuzingatia kwamba Wilaya ya Ngara iko pembezoni mwa Nchi, na inahitaji kupewa kipaumbele katika ajira.
Kuendelea kuelimisha wananchi, ili akinamama wajawazito waweze kuwahi vituo vya huduma ili kusaidiwa na kupunguza vifo vya wazazi.
Kuelimisha wajawazito kuwahi kuanza kliniki mapema ili kugundua matatizo kama upungufu mkubwa wa damu, kifafa cha mimba na kuzuia matatizo hayo.
Kuelimisha/kuhamasisha jamii ili kujiunga na CHF iliyoboreshwa na hivyo kuongeza kipato katika vituo vya huduma.
FEDHA ZA DAWA, VIFAA TIBA NA VITUENDANISHI VYA MAABARA JULAI 2017- JUNE 2018
CHANZO |
KILICHOPANGWA |
KILICHOPOKELEWA |
KILICHOTUMIKA |
SALIO |
HSBF
|
304,990,831.20 |
186,393,492.12 |
95,156,762.69 |
91,236,729.43 |
MSD
|
512,900,000.00 |
794,632,286.60 |
360,129,400.00 |
434,502,886.60 |
NHIF/CHF/USER FEE/RBF
|
265,772,623.71 |
167,205,884.00 |
167,205,884.00 |
0 |
NB. Fedha ya inayoonekana kama salio la HSBF ni fedha iliyolipwa MSD na dawa hazijaletwa, pia Tsh. 434, 502,886.60 ni salio la fedha zilizowekwa na Wizara katika account za vituo lakini pia kuna vituo vinavyodaiwa na MSD kwakuwa hawana pesa katika account zao. Vituo kwa sasa wanapokea dawa/vifaa tiba katika vituo vyao kwani wao ndiyo wanaonunua na kupokea kwa kupitia kamati za zao.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa