- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII.
Picha/Jina
|
CHEO
|
MAWASILIANO
|
Ndugu, Emmanuel Kulwa
|
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii (W)
|
+255 787 402 389
maendeleoyajamii@ngaradc.go.tz
|
Idara ya Maendeleo ya Jamii inafanya kazi zake kwa kuzingatia sera ya Maendeleo ya Jamii na pia miongozo mbali mbali inayotolewa na serikali. Katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 Idara ililenga kutekeleza mambo yafuatayo:-
MAFANIKIO
Katika kipindi cha Julai 2017 – Julai 2018 Idara imefanikiwa kufanya mambo yafuatayo;
Kutoa mikopo kwa fefdha za mapato ya ndani jumla ya T.shs. 30,000,000/= kwa vikundi 18, kati ya hivyo vikundi 11 vya wanawake na vikundi 07 vya vijana.
Usajili wa vikundi vya kijamii, kiuchumi, na VICOBA 100.
Kufanya ufuatiliaji kwa vikundi vilivyopata mikopo ili kutoa elimu ya ujasiriamali na kutatua migogoro inayotokea ndani ya vikundi ili kuweza kuboresha shughuli za vikundi na marejesho ya fedha za mikopo kwa muda uliopangwa katika kata 20.
Kuwezesha walengwa wa mpango wa TASAF kupata malipo yao ili kuwawezesha watoto wao kwenda shule pia wale walio chini ya miaka mitano kupelekwa kliniki na kuwapatia walengwa wa mpango ajira za muda na kuongeza vipato vya kaya katika vijiji 52.
Kuhamasisha kaya za walengwa wa mpango wa TASAF kutumia ruzuku wanazopata kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi ikiwemo ufugaji kuku, mbuzi, bata, kilimo cha bustani nk.
Vikundi vya ujariamali vya wanawake vinajitahidi sana kurejesha fedha wanazokopeshwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri ukilinganisha na vikundi vya vijana.
CHANGAMOTO
Katika utekelezaji wa shughuli za idara, changamoto mbali mbali zilijitokeza kama ifuatavyo:-
Upungufu wa fedha za bajeti iliyopangwa na idara. Idara ilitengewa fedha kidogo ambazo hazikutosheleza kufanya shughuli zilizokuwa zimepangwa kufanyika.
Ukosefu wa fedha kutoka kwa wafadhili hasa katika shughuli za kudhibiti UKIMWI, baada ya wafadhili kumaliza muda wao na kusababisha shughuli zilizopangwa kutotekelezwa.
Upungufu wa watumishi Idarani, hali inayosababisha Idara kuwa na mtumishi mmoja tu katika ngazi ya kata.
Vikundi vya vijana kutokuwa waaminifu na nidhamu ya fedha, baada ya kupewa mikopo hugawana fedha na kuhamia nje ya wilaya na kushindwa kurejesha fedha walizokopeshwa kwa muda uliopangwa.
MIKAKATI/ UTATUZI WA CHANGAMOTO
Halmashauri itenge fedha za kutosha kulingana na mahitaji ya Idara ili shughuli zote muhimu ziweze kufanyika.
Kuomba vibali vya ajira kwa watu wenye taaluma ya maendeleo ya jamii ili kukidhi mahitaji ya Idara.
Fedha 10% yaani 4% ya wanawake na 4% ya vijana na 2% ya walemavu kutokana na mapato ya Halmashauri iendelee kutengwa kila fedha inapopatikana.
Serikali itoe mwongozo mpya utaoiwezesha halmashauri kuvishtaki mahakamani vikundi vya wanawake, vijana na walemavu vitakavyoshindwa kurejesha fedha za mikopo kwa muda.
UTENDAJI KAZI TASAF JULAI 2017 - JUNI 2018.pdf
HALI HALISI YA MIKOPO YA 2016-2017 NA 2017-2018.pdf
HALI YA MIKOPO NA MAREJESHO MWAKA 2014-2015 HADI 2017-2018.pdf
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa