- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Bw. Enock Ntakisigaye
|
|
CHEO
|
|
MAWASILIANO
|
|
|
Kaimu Afisaelimu Sekondari
|
|
+255 786 767 114
elimusekondari@ngaradc.go.tz |
TAARIFA YA MAENDELEO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Utanguliza:
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ina jumla ya shule 29, kati ya hizo 23 ni za serikali na 6 ni za binafsi. Aidha miongoni mwa hizo kuna shule 5 za kidato cha tano na sita zikiwemo 4 za serikali na 1 ni ya binafsi hivyo kutimiza azima ya Serikali ya kila tarafa kuwa na shule ya kidato cha tano na sita. Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya walimu 470 kati ya hao walimu wanaofundisha masomo ya sanaa ni 395 na wanaofundisha masomo ya hisabati na sayansi ni 75. Jukumu kubwa la idara ya Elimu Sekondari ni kuhakikisha kuwa vijana wote wanaojiunga na masomo ya Sekondari wanahitimu na kufaulu kwenye mitihani yao ya mwisho.
UTEKELEZA WA MIRADI KWA MWAKA 2017/2018
Halmashauri ya wilaya kupitia idara ya Elimu Sekondari kwa mwaka ulioishia Juni 2018 ilitekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya bweni moja lenye thamani ya Tsh.191,618,752.16 lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 112 katika shule ya sekondari Muyenzi kwa ufadhili wa Mamlaka ya elimu Tanzania (TEA). Vilevile Halmashauri inaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa 4 katika shule za Rusumo B darasa 1, Ngara 1 na Nyamiaga madara 2 na kukamilisha maabara 22 za sayansi katika shule za Shunga,Rusumo,Kanazi, Kibimba,Ndomba, Mugoma na Bukiriro kwa Tsh.212,042,140.94 chini ya ufadhili wa Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
USAJILI WA WANAFUNZI MWAKA 2018
Usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waka 2018
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilipangiwa wanafunzi kidato cha kwanza 3813 kwa mwaka 2018 ikiwa sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote 3813 waliohitimu darasa la saba kwa mwaka 2018 kujiunga na shule za kutwa. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa, walioripoti ni wanafunzi 3564 Sawa na 93%.
Usajili wa wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2018
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilipangiwa na OR-TAMISEMI wanafunzi kidato cha tano 839 kwa mwaka 2018. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa, walioripoti ni wanafunzi 664 Sawa na 79% hadi sasa.
MAFANIKIO
Kuna baadhi ya mafanikio tuliyofikia;
CHANGAMOTO
Pamoja na mafakio tajwa Idara ya Elimu Sekondari inaendelea kukabiliana na changamoto kadhaa;
Mikakati ya Kuboresha Taaluma
Baadhi ya mikakati ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika mwaka 2018;
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa