- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi wa Ngara wanashughulika na ufugaji wa mifugo ya aina mabali mbali. Kuna ng’ombe kiasi cha 70,000. Baadhi ya wafugaji wanafungia ng’ombe ndani. Mfano wa Ngombe wanaofugiwa ndani ni kama Frisian chotara F1, F2 & F3 wa aina ya Boran. Wafugaji waliobaki wanafuga aina ya Zebu na Ankole ambao uzalishaji wao wa maziwa ni kati ya lita 1-3 kwa siku. Katika kilimo mchanganyiko wa Migomba-Kahawa wanayama wadogo kama mbuzi na kondoo hufugwa pamoja na ng’ombe wa maziwa. Maeneo ya nyanda za Chini Ng’ombe na mbuzi wanafugwa kwenye machugo huria. Samadi hutumika kama mbolea.
Ndikana kali, Ndigana baridi, Moyomaji, Mkojodamu ni magonjwa ya yaliyozoeleka. Ugonjwa wa Ndigana kali ndio unaouwa ng’ombe zaidi kuliko magonjwa mengine. Katika Misitu ya hifadhi kuna mbung’o wanaosababisha ugonjwa wa ndorobo(nagana) unaosababisha vifo vya ng’ombe pia. Milipuko ya ugonjwa wa Midomo na Miguu, Chambavu(koto), Mapele ngozi, hutokea pia na Chanjo dhidi ya magonjwa hayo hutumika kama njia ya kinga.
Aina ya wanyama wanaofugwa katika Wilaya ya Ngara ni kama ifuatavyo:
Fursa za Kiuchumi
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa