- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Asili /Chimbuko
Wilaya ya Ngara ni moja ya wilaya nane (08) za mkoa wa Kagera, Tanzania. Wenyeji wa Ngara ni Wahangaza na Washubi na wanaongea Kihangaza na Kishubi. Kabla ya kuitwa jina la Ngara, ilijulikana kama Kibimba yaani Pori. Chanzo hasa cha jina la Ngara ni sehemu iliyokuwa maalumu kwa mikutano, ambayo ilifanyika chini ya miti mikubwa inayoitwa iminyinya yingara. Hivyo, Mti wa umunyinya ulipandwa halmashauri ya wilaya ya Ngara kama kumbukumbu, kwani umebeba jina la wilaya ya Ngara. (Chanzo: https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-wilaya-ya-ngara-utamaduni-wa-wakazi-wa-ngara-na-chanzo-cha-jina-la-kabila-la-wahangaza.1193348/).
Eneo
Wilaya ya Ngara ina ukubwa wa eneo lipatalo 3,744 Km2, imegawanyika katika tarafa nne (4) ambazo ni Nyamiaga, Kanazi, Rulenge na Murusagamba, kata 22, vijiji 75 na vitongoji 389.
Watu wa Ngara
Wakazi wa wilayani Ngara wamegawanyika katika makabila mawili ambayo ni Wahangaza na Washubi. Kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2012 wilaya ina jumla ya kaya 63,293 zenye watu 320,056, ambapo kati ya hao 152,443 (47%) ni wanaume na 167,613 (53%) ni wanawake. Ongezeko la watu kati ya sensa ya mwaka 2002 na sensa ya mwaka 2012 ni asilimia 2.7
Hali ya Hewa
Wilaya ya Ngara ina misimu miwili ya mvua, yaani mvua za vuli na za masika. Vuli huanza mwezi Septemba hadi Desemba na masika huanza mwezi Februari hadi Mei. Kiwango cha mvua kwa mwaka hufikia wastani wa milimita 1400 kwa ukanda wa juu na milimita 800 kwa ukanda wa chini. Wastani wa joto kwa ukanda wa kusini ni 17 °C na ukanda wa kasikazini joto upanda hadi 25 °C.
Shughuli za Kiuchumi
Uchumi wa wilaya ya Ngara unategema shughuli za kilimo na ufugaji. Mazao makuu yanayolimwa ni kahawa, ndizi, mihogo, mahindi, maharage na mtama kwa upande wa mazao ya chakula. Mazao makuu ya biashara ni kahawa, ndizi na parachichi. Karibu asilimia 95 ya wakazi wa wilaya hii wanategemea kilimo kama chanzo cha mapato na shughuli za kilimo huchangia zaidi ya asilimia 94 ya pato la wilaya.
Orodha ya Viongozi
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa