- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HALI HALISI YA WATUMISHI WILAYANI NGARA.
PICHA/JINA
|
|
CHEO
|
|
MAWASILIANO
|
Bi. Sabra Mwakenja
|
|
Afisa Utumishi
|
|
+255 658 905 665
Email: utumishi@ngaradc.go.tz |
Halmashauri ya wilaya ya Ngara kwa sasa inao watumishi 2,249 wanaotakiwa ni watumishi 2,708 hivyo tunao5.1 Idadi ya watumishi Halmashauri ya wilaya ya Ngara
2.1. Idadi ya watumishi Halmashauri ya wilaya ya Ngara
No
|
Idara
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
Mahitaji
|
Pungufu
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
1
|
Utawala na utumishi
|
139 |
28 |
167 |
172 |
05 |
2
|
Fedha na Bihashara
|
15 |
6 |
21 |
27 |
6 |
3
|
Ujenzi
|
13 |
1 |
14 |
18 |
4 |
4
|
Maji
|
14 |
5 |
19 |
28 |
9 |
5
|
Elimumsingi
|
951 |
634 |
1585 |
2179 |
594 |
6
|
Elimusekondari
|
371 |
138 |
509 |
535 |
56 |
7
|
Maendeleoyajamii
|
13 |
6 |
19 |
37 |
18 |
8
|
Kilimo ushirika
|
35 |
20 |
55 |
111 |
56 |
9
|
Mifugo na Uvuvi
|
18 |
6 |
24 |
111 |
86 |
10
|
Sheria
|
1 |
0 |
1 |
2 |
1 |
11
|
Ugavi
|
2 |
3 |
5 |
5 |
0 |
12
|
Ufugaji nyuki
|
2 |
0 |
2 |
4 |
2 |
13
|
Teknolojia,habari,mawasilianona uhusiano
|
2 |
1 |
2 |
3 |
1 |
14
|
Ardhi na maliasili
|
8 |
0 |
8 |
15 |
7 |
14
|
Ukaguziwandani
|
2 |
1 |
3 |
4 |
1 |
16
|
Afya
|
110 |
232 |
342 |
600 |
257 |
17
|
UchuminaMipango
|
2 |
0 |
2 |
5 |
3 |
18
|
Uchaguzi
|
1 |
0 |
1 |
3 |
2 |
|
JUMLA KUU
|
1687 |
1073 |
2751 |
3869 |
1098 |
upungufu wa watumishi 459 sawa na 18.4% kama inavyoainishwa katika jedwali.
2.2.1. Mafanikio katika Sekta ya Utumishi na Utawala kwa kipindi cha mwaka July 2012 – Juni 2015.
• Halmashauri katika hali ya kuboresha mazingira kupitia idara ya utumishi na utawala imejenga ofisi za Kata 13 na ofisi za vijiji 31 Sambamba na ujenzi na ukarabati wa nyumba mbalimbali za watumishi.
• Idadi ya watumishi imeongezeka kutoka watumishi 2223 mwaka 2014 hadi watumishi 2770 mwaka 2015 sawa na ongezeko la 17.5%. mwaka wa fedha 2014/15 tumepata kibali na kuajiri jumla ya watumishi 34 wa kada za madreva, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja na makatibu mahususi.
• Serikali imeweza kulipa madeni mbalimbali ya watumishi yanayojumuisha malimbikizo ya Mishahara, uhamisho, likizo, matibabu na masomo kiasi cha Tsh 156,110,828.07. Mpaka julai 2015 bado kuna madeni ya jumla Tsh 167,864,000 madeni ya malimbikizo ya mishahara na uhamisho wa watumishi.
• Watumishi 346 wamepandishwa vyeo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 na tayari wamesharekebishiwa mishahara yao tangu mwezi april 2014 kupitia mfumo uliboreshwa wakushughulikia maslahi ya watumishi HCMIS (LAWSON).
• Halmashauri kupitia mpango wa mafunzo imeendelea kuimarisha ujuzi na taaluma za watumishi kujiendeleza katika fani mbalimbali walizo ajiriwa nazo kwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2015 watumishi 26 wamegharimiwa / wanagharimiwa katika vyuo mbalimbali hapa Nchini.
• Aidha Halmashauri katika kuboresha mazingira ya kazi inaendelea na ujenzi wa Ofisi ya Kata Rusumo.
2.3. CHANGAMOTO.
Upungufu wa watumishi katika Halmashauri hii unachangiwa na sababu zifuatazo:-
1. Hali ya kuwa na wasiwasi wa usalama katika Wilaya, ingawa kwa sasa hali ni nzuri. Hali hii kama ilivyokuwa inatangazwa na kuandikwa katika vyombo vya habari ilisababisha wataalam walioko sehemu mbalimbali nchini kuwa na wasiwasi wa kuishi hapa wilayani au kuja kufanya kazi katika wilaya hii.
2. Kutokana na umbali wa wilaya hii kutoka sehemu mbalimbali bidhaa na huduma muhimu za viwandani kama vile vinywaji, vifaa vya ujenzi, mavazi, mafuta na vipuri na huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinafanya bidhaa hizo kuwa ghali kulinganisha na maeneo mengine nchini. Hivyo watumishi wengi hasa wanaopata ajira kwa mara ya kwanza kutopendelea kufanya kazi Ngara.
2.4. MIKAKATI.
Katika kupunguza tatizo la watumishi Halmashauri ina mikakati ifuatayo:
1. Kuendelea kuomba vibali vya ajira za watumishi wapya toka Wizarani.
2. Kuimarisha ulinzi na usalama na kuwaeleza watu kuwa hali ya ulinzi na usalama imeboreka ili kundoa hofu miongoni mwa watu kuwa Ngara ni sehemu isiyo salama.
3. Kuendelea kuwasiliana na serikali kuu juu ya tatizo la upungufu wa watumishi na kuandaa mfumo wa motisha kwa watumishi wapya na waliopo na hasa wale wanao fanya kazi katika mazingira magumu.
MAMLAKA YA MIJI MIDOGO NGARA NA RULENGE.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara inazo Mamlaka mbili za Miji midogo ya Ngara na Rulenge. Mamlaka ya mji mdogo wa Ngara ilianzishwa mwaka 2008 na Mamlaka ya Mji mdogo wa Rulenge ilianzishwa Mwaka 2015
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa