- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Saturday 2nd, November 2024
@KATA YA MUGOMA,NGARA
Katika maadhimisho ya kilele cha kampeni ya Nyumba ni Choo wilayani Ngara iliyofanyika katika kata ya Mugoma siku ya Jumatano,05/06/2019,Mhamasishaji mkuu Mrisho Mpoto aliwaeleza wananchi wa Mugoma juu ya faida za matumizi bora ya choo kilicho bora au cha kisasa.
Mhamasishaji Mrisho Mpoto
Mrisho Mpotoo alisema,”Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inawataka watu wawe na choo Bora au kama una uwezo ujenge choo cha kisasa.Serikali inawakumbusha kuwa choo bora ni kile chenye kuta nne imara, kilichoezekwa juu kwa bati au nyasi kulingana na uwezo wa mwananchi kwa ajili ya kuzuia mvua kujaza shimo la choo.Pia choo bora lazima kiwe na mlango unaofunga ili kuwa na faragha kwa mtumiaji pamoja na kuzuia wadudu walukao na kutambaa wanaoweza kueneza magonjwa na kuhatarisha afya zetu.Mwisho choo bora kinatakiwa kuwa na mfuniko wa kufunikia tundu la choo pamoja na kuwa na sakafu inayoweza kusafishika pamoja na pomba la kutolea hewa chafu.”
Pia Mrisho Mpoto alitoa elimu ya hatua sahihi za unawaji mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni. Elimu hii aliitoa kwa vitendo ambapo wanafunzi walionesha kwa matendo hatua hizo mbele ya hadhara yote iliyokuwa imekusanyika.
Baada ya Mrisho Mpoto kutoa elimu juu ya kampeni ya usichukulie poa nyumba ni choo, Afisa Afya wa Wilaya ya Ngara Ndugu Salumu Kimbau alitoa ripoti ya Wilaya ambapo alisema ni asilimia 33.2 tu wanachi wa Ngara ambao wana vyoo bora na asilimia 66.8 ikiwa na vyoo visivyo bora.
Afisa Afya Ngara, Ndugu Salumu Kimbau
Pia alieleza changamoto zinaikumba idara ya Afya wilayani ngara ikiwemo; uchache wa wataalam wa Afya pamoja na uchache wa Vyombo vya usafiri ambavyo huwawea vigumu wao kutimiza majukumu yao kwa uharaka kama kutoa elimu na uhamasishaji pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara katika vijiji vya wilayani Ngara.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan J. Bahama alitoa shukrani zake za dhati kwa tume ya uhamasishaji wa Usichukulie poa nyumba ni choo kwa kuwakumbusha wanachi juu ya umuhimu wa kujenga na kutumia vyoo bora. Pia aliwaasa wanachi wote wilayani Ngara kuanza kujenga vyoo bora maana ni asilimia 33.2 tu katika hii ambao wana vyoo vilivyo bora ili kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, Ngara iwe na vyoo bora kwa asilimia 99 mpa 100.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngara, Ngugu Aidan Bahama J. Bahama
Mkurugenzi wa Wilaya alielezea pia changamoto zilizopelekea Wilaya ya Ngara kuwa na asilimia chache za watu wenye vyoo bora ikiwemo; Uwepo mdogo wa wafanyakazi wa Afya kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka Wilaya pia uwepo wa wazee na watu wasiojiweza ambao imewawea ngumu kuwa na vyoo bora vinavyotakiwa na serikali.
“Changamoto hizi huweza kutatuliwa kama hawa wafanyakazi wachache wataweza kuweka nia ya kuwaelimisha wananchi kuwa sasa ni zama za kuwa na vyoo bora na si bora choo.”Alisema Mkurugenzi.
Pia Mkurugenzi aliwaomba watendaji wa Vijiji kushirikiana na wananchi kaya kwa kaya na kuhakikisha kila kaya inatumia choo kilicho bora.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngara Ruten Kanali Michael M. Mntenjele alionesha kusikitishwa na asilimia kubwa ya wanachi wa Wilaya ya Ngara kutokuwa na vyoo bora. Aliwaomba Waheshima madiwani kuhakikisha wanashughulikia kaya ambazo hazina vyoo kabisa kuweza kujenga vyoo bora ndani ya muda mfupi ujao. Pia alitoa ahadi ya kuwa na vyoo bora wilayani Ngara kwa wananchi wake wote ndani ya muda mfupi kabla ya mwaka 2019 kuisha.
Mkuu wa Wilaya Ngara, Lt Col Michael M. Mntenjele
Pia Mkuu wa Wilaya aliwaasa wanachi akisema “kuzingatia matumizi ya choo bora ni wajibu wa kila mwanachi pamoja na kujenga vyoo bora kwa manufaa ya Afya ya kila mmoja wetu”.
Sherehe za maadhimisho haya ziliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa vikundi vya Ngoma,kucheza na nyoka pamoja na michezo ya sarakasi iliyovutia macho ya wananchi wengi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa