- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisa Kilimo na Ugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara wametakiwa kuachana na tabia ya kukaa ofisini, badala yake wamehimizwa kwenda vijijini kuwahamasisha wakulima, kuanza kuandaa mashamba tayari kwa kupanda mazao katika msimu huu.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele, ametoa wito huo wakati wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani, lililofanyika Agosti 29, 2018 katika ukumbi wa Halamshauri ya Wilaya ya Ngara.
“Kazi yaAfisa Kilimo na Afisa Ugani ni kwenda kwa wakulima, ili wawaelekeze namna bora ya kupanda mahindi, maharage na mazao mengine, ambayo mkulima anataka kuzalisha, na siyo kukaa tu ofisini.” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya Lt. Col. Mntenjele.
Msimu wa mvua umeanza kwa hiyo amewatakaka waheshimiwa madiwani, kuwahamasisha wananchi kuanza kupanda mazao, huku akimnukuu Mwalimu Julius K. Nyerere; kwamba mvua za kwanza ni za kupandia.
Amesema wakulima wengine wanatabia ya kusubiri, hivyo wanapotenza muda; matokeo yake wanapata mazao kidogo kwani mvua zinakoma kabla hawajavuna; huku akiwaomba waheshimiwa madiwani kuwahamasisha wananchi wazingatie maelekezo ya wataalamu.
Amewahimiza wataalamu wa kilimo kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuzingatia utaalamu wanaowaelekeza, na kuwatawataka wanachi kuachana na utaalamu uliopitwa na wakati wa kutumia mbegu zisizokuwa na tija.
“Mbegu zilizobora zipo madukani tuachane na mbegu zetu za asili, kwani mbegu za kisasa wanakwambia mbegu inakomaa muda gani, kwa hiyo inakupatia nafasi ya kuchagua ni lini unataka kupata mazao yako.” Alisema Lt. Col. Mntenjele.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa