- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuacha tabia ya kuwakaribisha wageni kutoka nchi jirani wanaokuja kufanyakazi, kwani hawawezi kujua aliyeathirika, na asiyeathirika kwa ugonjwa wa ebola.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele ametoa rai hiyo, wakati wa Baraza la waheshimiwa madiwani lililokaa Agosti 29, 2018, katika ukumbi wa Halamshauri ya Wilaya ya Ngara.
Aliliambia Baraza hilo kwamba tishio la ugonjwa huo ni kubwa, kwani mtu akishaambukizwa anakaa siku takribani 21 bila kuonyesha dalili yoyote ya ugonjwa huo, mnaweza kuona sasa umuhimu wa kuchukua tahadhari.
“Niwaombe ndugu zetu wenye tabia ya kuwaingiza wageni kwenye familia zetu, ili watufanyie kazi, akija ameambukizwa uwezi kuona dalili wala kujua; atakufanyiakazi siku chache kasha anaambukiza familia nzima.” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya Lt. Col. Mntenjele.
Amesema ugonjwa wa ebola mtu akiupata ana asilimia hamsini kupona na asilimia hamsini kupoteza maisha, na kuongeza kwamba hata vivyo asilimia hamsini ni kwa nchi zilizoendelea ambao wana miundimbinu mizuri ya matibabu.
Wakati huo huo, amelishukuru kwa kusimamia na kufuata maelekezo ya uandikishaji wa vitambulisho vya taifa, kwani zoezi hilo linaendelea vizuri ambapo takribani wananchi katika kata 18 wamejiandikisha kupata vitanbulisho hivyo.
Amezitaja kata za Kabanga, Mabawe, Mugoma na Kirushya kuwa hazijakamilisha zoezi hili, na kuongeza kwamba kuna taarifa zisizo rasmi, kwamba baadhi ya viongozi wamekuwa wakitaka kuwaandikisha wafanyakazi wa ndani kinyume cha utaratibu.
Amesema kitendo hicho ni kibaya sana, kwani kwa kufanya hivyo mnahatarisha mstakabari wa usalama wa nchi yetu, kwa sababu ukimuandikisha mrundi maana yake unamhalalisha kuwa ni mtanzania.
“Kwa hiyo ninaomba tuchukue tahadhari, kwa kutumia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, tutafanya ufuatiliaji tukijilidhisha, kwamba kuna watu wanaofanya hivyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.” Alisema Lt. Col. Mntenjele
Aidha, amewaomba waheshimiwa madiwani watoe elimu juu ya umuhimu wa kuwaandikisha watanzania pekee, huku akidai kwamba waandikishwe watanzania pekee wenye sifa za kupewa vitambulisho hivyo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa