- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wanawake Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, baada ya baadhi ya wanawake hao, kuwaua au kuwatelekeza watoto hao katika mazingira hatarishi baada ya kujifungua.
Wito huo umetolewa na mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya National Microfinance Bank tawi (NMB) la Ngara mkoani Kagera Bi Witness Mwanga, wakati walipotembelea kituo cha watoto yatima cha ANGEL'S HOME kinachosimamiwa na Kanisa katoliki Rulenge wilayani Ngara.
"Sisi tungetelekezwa au kuuawa leo tusingeliweza kuwatembelea watoto hawa, wanaohitaji msaada mkubwa, wito wangu kwa wazazi ogopeni Mungu na mamlaka zilizo juu yenu kwa kuwapa watoto haki ya kuishi" Alisema Bi. Mwanga.
Bi Mwanga amesema kuzaa mtoto ni Baraka; hivyo mtoto anahitaji malezi, matunzo na kupewa haki zake za msingi, kuliko kumtupa au kumsababishia maisha magumu kwa kulelewa na watu wengine.
Ndugu Meleck Manyama amevitaja vitu vilivyotolewa na wafanyakazi wa NMB tawi la Ngara wametoa msaada wa vyakula, vinywaji, mavazi, sabuni, mafuta ya kupikia na vifaa vya kujifunzia kwa wanaosoma, vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 340,000.
Ndugu Manyama amesema wao kama sehemu ya jamii, wamechangishana na kupata kiasi hicho kisha kuungana na watoto hao kwa kuwapatia gawio la mapato kama sadaka yao kwa kuuanza mwaka mpya 2019.
"Mazingira tuliyoyaona watoto hao wanahitajika msaada zaidi, kutoka kwa watu wenye mapenzi mema ili viwasaidie na kuwatia moyo walezi wao, ambao ni masista wa kanisa kanisa Katoliki na kwa jinsi wanavyowahudumia Mungu awabariki" Amesema Manyama
Nao watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Angle's home wametoa Shukrani zao kwa zawadi walizopokea huku wakinyanyua mikono kuwaombea kwa Mungu wakijawa na furaha,wakicheza na kuimba.
Aidha, mkuu wa kituo hicho Sr. Mariagholeth Felix amewashakuru wafanyakazi wa Benki ya NMB na kuongeza kwamba watoto wanaolelewa kituoni hapo ni wenye umri wa miezi sita hadi miaka 20 ambao walipatikana baada ya mama zao kufariki kwa kujifungua au kuokotwa.
Sr. Felix amewashukuru pia watu mbalimbali wanaofika kutoa msaada kwa watoto katika kituo hicho, huku akisema kwamba kituo hicho kwa sasa kina watoto wapatao 47 wanaotoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa