- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Afisa Elimu Mkoa wa kagera Mwl Michael Ligola akiongozana na Maafisa Elimu taaluma Mkoa Mwl Oscar Msabaha, Mwl. Simon Chibon na Afisa Michezo Ndg Kepha Elias amefanya ziara Wilayani Ngara
Lengo la ziara hiyo ufuatiliaji shuleni na kufanya Kikao kazi na Maafisa Elimu Msingi sekondari , TSC, Uthibiti ubora , Utamaduni michezo .Walimu Wakuu shule za Msingi, Maafisa Elimu Kata na walimu Wakuu shule za Msingi.
Afisa elimu mkoa Mwl Ligola ametembelea shule za msingi Ngara mjini, Murgwanza, Mumiterama na shule za sekondari Murgwanza na Mumiterama
aidha amepongeza ujenzi wa vyumba vya madarasa mazuri yaliyojengwa shule ya msingi Ngara mjini pia Mumiterama sekondari
Afisa Elimu elimu mkoa Mwl Michael Ligola baada ya ziara ya kutembelea shule za msingi na sekondari alifanya kikao kazi katika ukumbi wa Ngara sekondari uliopo Ngara mjini.
Washiriki wakiwa ni maafisa wote ngazi ya wilaya elimu msingi, sekondari ,TSC, Uthibiti ubora na utamaduni michezo.pamoja na walimu wakuu wa shule za msingi , maafisa elimu kata na wakuu wa shule.
Afisa elimu mkoa alisisitiza mkakati ifuatayo ya kuinua taaluma shuleni
Afisa Elimu Mkoa Mwl Michael Ligola akiongea katika Kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Ngara Sekondari.
Afisa Elimu Sekondari Mwl Enock Ntakisigaye akiwakaribisha viongozi walioongozana na Afisa Elimu Mkoa wa kagera Mwl Michael Ligola.
Maafisa Elimu Kata , Wakuu wa shule na walimu Wakuu shule za Sekondari wakiwa kwenye Kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Ngara sekondari.
Maafisa wa wilaya Kutoka Elimu Msingi , Sekondari, TSC, Kuthibiti Ubora wa shule na utamaduni michezo.
waliokaa mbele Maafisa Elimu Kata 22 Wilayani Ngara wakiwa kwenye Kikao kazi.
Afisa michezo Mkoa kagera alipotembelea kiwanja Cha michezo shule ya Msingi Ngara Mjini wakati wa ziara ya Afisa Elimu Mkoa Kutembelea shule hiyo.
Afisa elimu mkoa Mwl Michael Ligola akiongea na Wazazi shule ya Msingi Ngara mjini.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa