- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WILAYANI NGARA
Afisa elimu Msingi Bi Josline Bandiko ambaye ameongoza timu ya Maafisa Elimu Utawala kufanya zoezi la ufuatiliaji Ufundishaji shule za Msingi.
Ambapo Leo wametembelea shule Mpya ya Msingi ( Nyaihanga) , kumunazi ziliyopo kata ya Kasulo Tarafa ya Nyamiaga .na Shule Mpya ya Msingi Chamabale kata ya Nyakisasa Tarafa ya Rulenge.
Lengo ni ufuatiliaji wa ufundishaji shuleni,na Usajili wa wanafunzi Darasa la kwanza.
Aidha Afisa Elimu Msingi Amesema pamoja ufuatiliaji shule zenye wanafunzi Darasa la 1 Hadi VII pia kuzitembelea shule Mpya zilizojengwa 2023 na kusajiliwa ambazo zimepokea wanafunzi kuanza Darasa la 1 2024.
Kuwepo Kwa shule hizo kumeondoa adha kubwa waliyokuwa wakiipata wanafunzi kutembela umbali Kilometa 10 Hadi 16 kufuata shule ilipo ambapo matokeo yake kushindwa kuendelea na masomo.
Mwisho Afisa elimu Msingi Bi Josline Bandiko Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa vyumba vya Madarasa pia Ujenzi wa Shule Mpya za Songambele, Nyaihanga, Chamabale, Mkalela na Nyanza ambazo zimesajiliwa na kupata namba za usajili na Sasa kupokea wanafunzi 2024; Nyumba za walimu na Ujenzi wa Matundu ya vyoo.
Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi mpya Nyaihanga kata ya Kasulo Tarafa ya Nyamiaga wilayani ngara.
Wanafunzi wakiwa wamefika shuleni.
Nyumba za Walimu 3 ni 1 Chambale Shule ya Msingi Mpya.
Maafisa wakiikagua nyumba ya walimu.
Shule ya Msingi Chambale( shule Mpya) tayari imeshapokea wanafunzi.kuanza Darasa la kwanza.
Shule ya Msingi Chamabale iliyopo kata ya Nyakisasa Tarafa ya Rulenge.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa