- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 21/11/2023 kimefanyika kikao Cha walimu wakuu wa shule za msingi 128 wamehudhuria kikao Kilichofanyika ukumbi wa community centre Ngara Mjini.
Mgeni Rasmi katika kikao hicho alikuwa Afisa Elimu Msingi Bi Josline Bandiko.
Mkiti wa walimu wakuu Mwalimu Alfredy Mabagara Alimpongeza Afisa elimu Msingi Kwa ushirikiano na ofisi ya Idara ya Elimu
Mgeni Rasmi Bi Josline Bandiko Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Ngara alisisitiza katika kikao hicho kuwa Kila Mwalimu Mkuu kutimiza wajibu wake, kusimamia Miradi iliyoko shuleni kwake, kusimamia ufundishaji shuleni, kuhakikisha usajili wa wanafunzi unafanyika kwa umakini mkubwa, Ufundishaji Kusoma ,kuandika na kuhesabu( KKK)asiwepo mwanafunzi wa kuingia Darasa la 3 bila kujua Kusoma ,kuandika na kuhesabu( KKK), pia shughuli zote za Shule .
Nae Afisa utamaduni/michezo Bi Elina patrice alisisitiza uzingatiaji shuleni Nyimbo za uzalendo, paredi pia kuendelea na maandalizi ya michezo ya shule za Msingi UMITASHUMTA 2024.Aidha amesema Wilaya ya Ngara Mkoa wa kagera imepata mchezaji mmoja Dorice Mbonimpa kutoka shule ya Msingi Nyamiaga kuchaguliwa timu ya taifa Mpira wa kikapu under 14 wasichana kitaifa.
Mgeni Rasmi Afisa elimu Msingi Bi Josline Bandiko akiongea katika kikao Cha walimu wakuu wote wilayani Ngara kagera
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa