- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan John Bahama, amewataka wataalamu wanaopima ugonjwa wa Ebola katika mipaka ya Rusumo, Kabanga na Murusagamba, kuhakikisha wageni wanaoingia nchini wanapimwa ugonjwa wa Ebola.
Mkurugenzi Mtendaji ndugu Bahama amesema hayo Mei 23, 2018, alipotembelea vituo hivyo, ili kujiridhisha na zoezi la kupima ugonjwa wa Ebola.
Ameambiwa kwamba zoezi linaendelea vizuri, lakini wafanyakazi wanakabiriwa na changamoto ya baadhi ya wageni kupita njia za panya na kukwepa kupita kwenye vituo vya kupima ugonjwa wa Ebola.
“Hakikisheni kila mgeni anayeingia anapimwa, kwani tusipowapima wanapoingia nchini, tunaiweka nchi yetu katika janga la ugonjwa wa ebola, wakati tuna vifaa vya kukutosha kufanyakazi hiyo.” Alisema Ndugu Bahama.
Amewataka kuchunguza na wakibaini kuwa wanaokwepa ni wengi wampe taarifa, ili aweze kuvishirikisha vyombo vya ulinzi na usalama viweze kusaidia katika kuwabaini wanaokiuka utaratibu.
Aidha, Afisa Afya Mfawidhi wa Kituo cha Rusumo Dr. Stanley Chipasula, amemhakikishia Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bahama, kwamba hadi jana saa kumi na mbili jioni, hakuna mtu aliyebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola.
Ameongeza kwamba pamoja na kuwa na vitendea kazi vya kutosha, bado wanakabiriwa na changamoto ya upungufu wa wafanyakazi, kwani hadi sasa wapo wafanyakazi wawili pekee, wakati wageni wanaoingia nchini ni wengi sana.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa