- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mtoto Anthony Petro (10) wa kijiji cha Ngundusi katika Halamashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, alipokelewa Aprili 09, 2018, katika shule ya Amani Vumwe English Medium Pre-Primary and Secondary School wilayani Mwanga Kilimanjaro, kwa ajili ya kuanza masomo ya elimu ya msingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilayani ya Mwanga Ndugu Golden Ally Mgonzo, alimvisha Anthony mataji ya maua, kuonesha upendo na jinsi wananchi wa wilaya hiyo wanavyomthamini.
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Mwanga ndugu Mgonzo alimutakia mototo Anthony Amani, upendo, na baraka tele katika masomo yake na kumuombea Baraka za Mwenyezi Mungu zimtangulie katika maisha yake mapya.
Alisema mtoto huyo amekuwa na ujasiri, utiii, heshima, adabu, juhudi na hasa ya kuitunza familia bila kuwa na ubinafsi au uchoyo.
Akitumia mfano wa yai lililozama ndani ya maji, Mkurugenzi huyo aliwaonesha watu kuwa, Anthony alizama katika dimbwi la umaskini, ambapo kwa ujasiri wake ameibuka aikwa tunu katika familia.
"Tutahakikisha kipaji chake kinalindwa kwa weledi mkubwa, na kuelekeza kile kitakachokuwa matamanio yake katika maisha." Alisema Mgonzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ndugu Aidan John Bahama, aliwashukuru wakazi wa Mwanga na mmiliki wa shule hiyo, kwa mapokezi mazuri, ambayo hakuyatarajia.
Alisema baada ya Anthony kupokelewa shuleni hapo, anakwenda kuwatafuta wahisani watakaosaidia kuwasomesha dada zake, na kuongeza kuwa mmiliki wa shule ya Rusumo New Vision English medium ameonesha nia ya kuwapokea shuleni kwake.
Naye Afisa Elimu idara ya Msingi wilayani Mwanga ndugu Allan Saidi, alisema mtoto huyo ataishi katika mazingira salama na uangalizi mkubwa, ili aweze kutimiza azima yake.
Alisema idara yake itakuwa ikiratibu maendeleo ya taaluma na mahitaji yake, kama yataweza kupungua Halmshauri kupitia idara hiyo, itawajibika kusaidia kutatua changamoto za kiafya, kimwili na hata za kiakili.
Aidha, Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara ndugu Mussa Balagondoza, alimkabidhi mtoto Anthony kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Mwanga ndugu Alex Kameo, akwaomba kuwa karibu na mtoto huyo.
Alisema kama shule itamtumia katika udadisi alio nao, akapata taaluma ya darasani, ataweza kufanya mambo makubwa, wasiyotegemea kwani anao upeo mkubwa.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa