- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Mali ya Asili na Utalii Mhe. Dr. Hamis Kigwangala amewagiza askari wa wanyama pori nchini kuwa na makazi yao na ofisi zao katika mapori ya hifahdi ili kuweza kudhibiti ujangili na uvamizi katika mapori hayo.
Waziri Kigwangala ameyasema hayo ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Februari 28, 2018 wakati wa ziara yake wilayani humo kwamba ujangili na uvamizi wa mapori hayo unatokea kwa sababu askali hao wanaishi mjini.
“Sasa tubadilike tujenge nyumba na ofisi za askali hao katika mapori ya hifadhi ili tuweze kukabiliana na watu wanaoingia maporini kinyume cha sheria.” Alisema Waziri Kigwangala.
Aidha, amesisitiza kuwa askali hao wanatakiwa kuwa waadilifu katika majukumu yao na watakaokiuka agizo hilo itabidi sheria ichukue mkodo wake ili iwe fundisho kwa wengine.
Akitoa taarifa kwa Waziri Kigwangala mkuu wa wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele amesema hakuna barabara katika mapori ya hifadhi hali inayopelekea kushindwa kudhibiti ujangili na uvamizi katika mapori hayo.
Waziri Kigwangala amesema kuwa changamoto hiyo iko katika mapori mengi ya akiba hasa katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa na kuongeza kuwa wazo hilo atalifanyiakazi kwani bila kuwepo udhibiti wa waarifu hao mapori ya hifadhi yatavamiwa zaidi.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa