- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Ngara limemalizika jana tarehe 28/4/2017. Katika Baraza hilo la madiwani yapo mambo ya msingi ambayo yalijadiliwa. Mojawapo ya mambo ya msingi ambayo yalijadiliwa ni namna ya kuongeza mapato katika Halmashauri yetu ili shughuli za kimaendeleo ziweze kufanyika kwa wakati. Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni diwani wa kata ya Bukiriro mh. Erick Nkilamachumu aliongeza kuwa iwapo mapato ya Halmashauri yataongezeka basi hata zile asilimia kumi (10%) kwa ajili ya wanawake na vijana zitaweza kutolewa kwa wakati na kwa usahihi kama maagizo ya serikali yanavyotaka. Jambo jingine la msingi ambalo liligusiwa katika Baraza hilo la madiwani ni ushirikishwaji wa wananchi katika ufanyaji wa maamuzi lakini pia hata katika Baraza la madiwani lenyewe ili waweze kufahamu mambo ya msingi ambayo yanaendelea katika Halmashauri yao.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa