- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kikao cha Baraza la Madiwani kimefanyika Leo Tarehe 7/03/2023 katika Ukumbi wa Halmashauri .
Baraza limepitisha RASIMU ya Bajeti 2023/2024 inakisia kukusanya na kutumia Jumla ya Tsh 43,039,930,754.00 sawa na ongezeko la Asilimia 10.28
Ambapo Tsh 5,609,874,950.00 zinatokana na Mapato ya ndani sawa na ongezeko la Asilimia 48.94 ,Tsh 23,305,575,000.00 za Mishahara ya Watumishi sawa na Bajeti ya 2022/2023 Tsh 956,615,000.00 za Ruzuku Toka Serikali kuu (matumzi ya kawaida) na Tsh 13,167,865,804.00 fedha za Ruzuku ya miradi ya Maendeleo Toka Serikali kuu.
Aidha Halmashauri inatarajia kutumia Tsh 1,945,198,780.00 ikiwa ni asilimia 40 ya Mapato yasiyofungiwa Ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga Kutoa huduma za kijamii pamoja na ile ya uwekezaji katika sekta ya uchumi Kwa lengo la kuongeza Mapato ya Halmashauri .
kiasi chaTsh 2,877,819,090.00 ikiwa ni aslimia 60 ya Mapato yasiyofungiwa yatatumika Kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa kawaida.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa