- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Mkutano wa Baraza la Madiwani limefanyika katika Ukumbi wa Community Centre Ngara Mjini mkutano huo umeongozwa na Mhe. Wilbard Bambara Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya pia Ndg Josephat Sangatati kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya.
Mkutano huo humehudhuriwa na Makamu Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mhe. Adronizi Burindoli, Waheshimiwa Madiwani , Mkiti wa CCM Wilaya Cde. Vitaris Ndailagije katibu CCM Bi Anastazia Amasi Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndg. Mathias Mugatha, kamati ya Usalama, Wataalam wote Kutoka Halmashauri.
Maswali ya papo Kwa papo yaliulizwa na Waheshimiwa Madiwani ambapo Mhe. Sitini Rugina aliuliza Kwa kuwa katika kipindi Cha robo ya pili. October - Desemba 2023/2024 kulikuwa na mvua za Elinino na mvua hizo ziliharibu Barabara za Muhweza, Mukarehe ,Remela, Mukibogoye na Murukatilo - Mukarehe kupitika Kwa shida, Lini Barabara hizo zitatengenezwa licha ya kwamba waliahidiwa Barabara hizo zingetengenezwa katika kipindi hicho na kuwa zabuni ya utengenezaji imefunguliwa tarehe 21/2/2024 Swali hilo lilijibiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kuwa ni kweli Barabara hizo zilitangazwa Kwa ajili ya kupata mkandarasi Hadi kufikia tarehe 15/04/2024 Barabara hizo zitakuwa zimepata mkandarasi wa kuzitengeneza na kazi zitaanza.
Mhe safari Banigwa Diwani Kata ya mabawe aliuliza Mradi wa maji Kabanga - Mabawe unaojengwa Kijiji Cha kumwuzuza utaanza kuhudumia lini wananchi na wanafunzi wa Mabawe Sekondari na Jamii yote ya kumwuzuza Swali hilo lilijibiwa na Meneja Ruwasa Kuwa Mradi wa maji Kabanga umeanza Kutoa huduma upo kwenye muda wa matazamio utakaoisha Desemba 2024 Bomba kuu la kusafirisha maji limepita baadhi ya Maeneo ya Kijiji Cha kumwuzuza na Sasa Ruwasa inatafuta fedha za kusambaza maji kwenye Maeneo yaliyobaki katika Kijiji Cha kumwuzuza. Aidha Kwa shule ya sekondari Mabawe inashauriwa kuwekewa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kama Mpango wa muda mfupi wa kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji Kwa wanafunzi.
Mhe Yusuph katura aliuliza madai ya fedha za mzabuni Ndg Ally Suleimani zaidi ya Tsh 1,000,000 Kwa ajili ya ujenzi wa choo kituo Cha afya Lukole. Swali limejibiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kuwa kweli fundi alijenga vyoo kupitia Mradi wa Wash na pesa ziliisha kabla ya Mradi kukamilika kwani ni muda mrefu na uongozi wa kituo umebadilishwa fundi huyo awasilishe viambatisho vya madai yake.
Mhe Evance Magambo Diwani Kata ya kibimba alisema kwenye ziara ya Mkuu wa wilaya, na Mhe Mbunge wa Ngara walipokea kero mbalimbali miongoni mwa kero hizo ni pamoja na uchakavu wa majengo ya shule ya Msingi Ruganzo na kumutana shule hizi zinahitaji ukarabati mkubwa kwani zilianza mwaka 1955 na hazipo katika hali nzuri. Je lini Serikali itawekeza nguvu katika ukarabati wa shule hizo, Swali lilijibiwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya alisema shule hizo zinahitaji ukarabati mkubwa wa ujenzi wa Madarasa mapya. Ujenzi wa vyumba vipya katika shule kongwe unafanyika kulingana na Bajeti ya Serikali. Kwa kuwa shule hizi zipo katika orodha ya shule kongwe za Wilaya tuendelee kusubiri utekelezaji Toka Serikali kuu. Aidha Mkurugenzi alitaja shule kongwe zilizonufaika ni Mursagamba, Bukiriri, Kanazi, Ngara Mjini, muyenzi na kanyinya zote za Msingi. Aidha Kwa Ngazi ya Halmashauri kupitia Bajeti Bajeti ya Mwaka 2024/2025 Kwa kutumia mapato ya Ndani shule za Kata ya kibimba ikiwemo kumutana imepangiwa matundu 7 ya vyoo.
Baada ya maswali ya papo Kwa papo zilipokelewa na kujadikiwa taarifa Kutoka Kwa wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri ambazo ni kamati ya Utawala na Mipango, kamati ya Kudhibiti UKIMWI (CMAC) , Kamati ya Elimu na Afya, kamati ya uchumi, ujenzi na Mazingira pia Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo robo ya pili Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 , Taarifa za kiutumishi.
Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye Baraza lililofanyika tarehe 27/3/2024 katika Ukumbi wa Community Centre Ngara mjini.
Mkiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara akiwa na Makamu Mkiti Halmashauri Mhe Adronizi Burindoli katika mkutano wa Baraza.
Waheshimiwa Madiwani katika Baraza.
Mhe Erick kilamachum katika Baraza.
Waheshimiwa Madiwani katika Baraza lililofanyika Ukumbi wa Community Centre Ngara mjini.
Mhe Wilbard Bambara Mkiti wa Halmashauri ya Wilaya akihitimisha katika mkutano wa Baraza la Madiwani.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa