- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imewekeza shilingi bilioni 80 kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa umeme vijijini mkoani Kagera.
Hayo yameelezwa leo Septemba 27, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy wakati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipokuwa akiwasha umeme Kijiji cha Mubaba na Kijiji cha Nyantakara vilivyopo Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera.
“Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini ndani ya Mkoa wa Kagera imewekeza shilingi bilioni 80 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza umeme vijijini, na hivi ninavyoongea ndani ya mkoa huu kuna miradi mitano inatekelezwa,” amesema Mhandisi Saidy.
Ametaja miradi inayotekelezwa mkoani humo kuwa ni pamoja na mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, mradi wa kupeleka umeme pembezoni mwa miji, mradi wa ujazilizi, mradi wa kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na mradi wa kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji.
Mkoa wa Kagera una jumla ya vijiji 662, ambapo vijiji 512 sawa na asilimia 77.3% vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali ikiwemo REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza.
Wakala wa Nishati vijijini umeendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Kagera ikiwa na lengo la kuwapatia huduma za nishati wananchi ili kuboresha huduma za jamii maeneo ya vijijini na vijiji-miji.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa