- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mawaziri wa Sekta ya Madini wa Burundi Mh. Eng. Ibrahim Uwizeye na Tanzania Mh. Anthony Mavunde wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kwenye sekta ya madini ili kukuza mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi mbili hizi.
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika Jijini Bujumbura - Burundi na kuhudhuriwa na watalaamu wa nchi zote mbili.
Maeneo ya Ushirikiano yanajumuisha;
Akitoa maelezo ya awali Waziri wa Maji,Nishati na Madini wa Jamhuri ya Burundi Mh. Eng. Ibrahim Uwizeye amesema nchi ya Burundi
na Tanzania zimekuwa na urafiki wa muda mrefu na mahusiano mazuri,hivyo ni muhimu kutumia fursa hii kushirikiana kwenye sekta ya madini ili sekta hii itoe mchango unaostahili katika kukuza maendeleo ya Uchumi wa Burundi na Tanzania chini ya uongozi imara wa marais Mh. Evariste Ndayishimiye (Burundi) na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan (Tanzania)
Akizungumza katika hafla hiyo ,Waziri wa Madini wa Tanzania Mh. Anthony Mavunde amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na Burundi katika kuiimairisha na kuiboresha sekta ya madini ya nchi hizi mbili kwa kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa na kutumia fursa hii kuwaalika wachimbaji wa Nickel,cobalt na copper kutumia huduma ya Kiwanda cha Usafishaji madini ambacho kitajengwa katika eneo la ulipokuwa Mgodi wa Buzwagi ,Wilayani Kahama-Shinyanga.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa