- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wazazi katika Hamashauri ya Wilaya ya Ngara, wametakiwa kuchangia chakula kitakachotumika siku ya ugawaji wa dawa za minyoo na kichoho shuleni tarehe 6 Julai 2018, huku wakisistizwa kutowaruhusu watoto hao, kupata chakula hicho majumbani mwao, ili walimu waweze kusimamia zoezi hilo.
Hayo yamesemwa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Dr. Revocatus Ndyekobora Julai 03, 2018; wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya jinsi ya kugawa dawa hizo kwa watoto wa shule za msingi wilayani humo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
“Nawaomba wazazi na walimu mhakikishe watoto wote wenye umri kati ya miaka 05 – 14, wanahudhuria bila kukosa shuleni, ili waweze kupata dawa za kuwatibu magonjwa ya minyoo pamoja na kichocho.” Amesema Dr. Ndyekobora.
Amewataka wazazi wachangie chakula cha kutosha na kiandaliwe shuleni, ili watoto hao waweze kula chakula hicho chini ya usimamizi wa walimu watakaohakikisha kila mtoto atakayepata dawa hizo hakuna madhala yatakayojitokeza.
Aidha, amefafanua kwamba dawa za minyoo zitamezwa asubuhi, kwa sababu watoto inabidi wazimeze kabla ya kupata chai au chakula chochote; huku dawa za kuzuia kichocho watazimiza baada ya kula na kushiba.
Dr. Ndyekobora amesema wamevuka lengo walilojiwekea kitaifa mwaka 2017, kwani walilenga kutoa dawa kwa watoto 79, 156 wakaandikishwa watoto 77,869 na kufanikiwa kuwafikia watoto 68,584 sawa na asilimia 86.2%; mwaka 2018 wamelenga kuwapata watoto wapatao 80,000.
Hata hivyo, Mganga mkuu huyo ameiomba serikali kutafuta utaratibu wa kutoa dawa hizo kwa watoto pasipo kutegemea wafadhiri, kwani wafadhiri wanaposhindwa kutoa fedha hizo kwa wakati, zoezi linazorota na kusababi waathirika kupata matatizo zaidi.
Amewakumbusha baadhi ya wazazi wanaozembea kuchangia chakula siku ya utowaji wa dawa hizo, kuacha tabia hiyo kwani inakwamisha zoezi hilo, na kuwakatisha tamaa wazazi wenye moyo wa kuchangia, pamoja na kukwamisha juhudi za serikali katika kutokomeza magonjwa hayo.
Mganga mkuu huyo amesema anatambua ushikiriano na msaada mkubwa walipupata kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza zoezi hilo.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa