- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“Mheshimiwa Mkurugenzi chukua hatua kwa wakuu wote wa shule za sekondari waliopewa fedha za kukamilisha maabara na hawajakamilisha shughuli hiyo, hatuwezi kuvumilia wakuu wa shule wanaokwamisha utekelezaji wa shughuli za serikali.” Aliagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele.
Lt. Col. Mntenjele alitoa agizo hilo wakati wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani, lililofanyika Agosti 29, 2018 katika ukumbi wa Halamshauri ya Wilaya ya Ngara kufuatia tuhuma zilizotolewa na waheshimiwa madiwani kuhusu maabara za shule ya Kanazi na Murugwanza kujengwa chini ya kiwango.
Amesema kwamba katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali changamoto haziwezi kukosa, akawaagiza waheshimiwa madiwani kusimamia kwenye maeneo ambayo yana changamoto ili isije kuonekana hata viongozi ni sehemu ya kukwaza kazi hizo.
Akitoa mfano, Lt. Col. Mntenjele amesema shuele ya sekondari ya Kanazi imepewa milioni 19 ya kukamilisha maabara, lakini kilichofanyika pale ni sawa na ziro na kwamba shule za sekondari nyingine zimefanyakazi nzuri kwani maabara zao aimekamilika.
“Ukienda katika shule nyingine zilizopewa fedha za kukamilisha maabara zinapendeza unaona kweli kazi imefanyika, na kwa kweli unasema kama watoto wakishindwa mitihani yao ya sayansi anakuwa ni yeye mwenyewe kwani mazingira yanaruhusu watoto wasome.” alisema Lt. Col. Mntenjele
Alisema hatutaeleweka kama serikali inaleta fedha kwa ajili ya kufanyakazi, halafu kazi haionekani, inasikitisha sana na kuongeza kwamba uzembe huo unawakwamisha watoto kufanya vizuri.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan J. Bahama ametekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael Mntenjele kwa kuwaagiza Mkaguzi wa Ndani na TAKUKURU kufanya ukaguzi katika shule ya sekondari za Kanazi na Murugwanzi.
Amewataka kukagua kwa kina matumizi ya fedha waliyopewa katika hizo na wamletee ripoti; “Nendeni pale kagueni matumizi ya fedha iliyotolewa kisha mniletee ripoti nikishapata taarifa zote mbili nitazisoma kasha nitachukua hatua stahiki.” Alisema ndugu Bahama
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Erick Nkilamachumu amesisitiza kwamba mkaguzi wa ndani na ofisi ya TAKUKURU wamepewa kazi ambayo inabidi waifanye haraka iwezekanavyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.
“Mmepewa kazi tusaidieni kama mtu amepewa milioni tano basi kazi iwe ya milioni tano siyo mtu anapewa milioni tano kazi hata haishabiiani na kiwango cha fedha alichopewa.” alisema Ndugu Nkilamachumu.
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa