- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara - Leo
Mkuu wa Wilaya Mhe Col Mathias J Kahabi ameendelea na zoezi la Oparation Sikiliza na kutatua kero katika Wilaya ya Ngara.
Mkuu wa Wilaya aliongozana na kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Constantine Msemwa, kamati ya Usalama Wilaya, Waheshimiwa Madiwani Mhe Yusuph katura na Mhe Zawadi Diwani viti Maalum Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Maji (RUWASA) Umeme (TANESCO), mratibu wa vitambulisho vya taifa Wilaya NIDA , TARURA pia uongozi wa Kata.
Mkutano huo umefanyika Kijiji Cha Ngoma kata ya kasulo Tarafa ya Nyamiaga.
Kero kubwa ikiwa ni mfugaji Ndg Method kujimilikisha eneo la kufugia Kwa madai alipewa eneo na serikali ya Kijiji jambo ambalo iimeonekana si kweli.
Ambapo changamoto hiyo imetatuliwa na chama Cha wafugaji na wote watatumia eneo hilo bila kubuguziwa au kubaguana.
Aidha imetatuliwa kero baina ya wafugaji na Wakulima Ambapo Kila mfugaji ameahidi kulimaliza endapo linapotokea Ng'ombe amekula Mazao ya Mkulima watakuwa tayari kulipa.
Limefanyika zoezi maalum la Uchangiaji Ujenzi wa choo Cha shule ya Msingi Ngoma Ambapo imechangwa Tsh 1,500,000 ikiwa ni kero katika shule hiyo cash zilizochangwa tsh 220,000 na ahadi 1,280,000/ zimeahidiwa kulipa ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe ya Mkutano huo.
Wananchi wa kata hiyo wamefurahishwa na kumpongeza Kwa zoezi la Mhe Mkuu wa Wilaya la kusikiliza na kutatua kero.
Ss
Wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero uliofanyika Kijiji Cha Ngoma Kata ya Kasulo.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa