- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Tarehe 06/5/2024.
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara, akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalam, Wananchi na baadhi ya Wazee Maarufu wa Kata ya Kabanga walifanya Ukaguzi wa Ujenzi wa barabara unaosimamiwa na TARURA - Ngara.
Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa TARURA - Ngara, Eng Magori alisema mradi huo una urefu wa Mita 200 na utagharimu zaidi ya Tshs million 83 na hadi sasa Mkandarasi DEKA Enterprises co.Ltd amelipwa kiasi cha Tshs million 21 ambapo kulingana na Mkataba Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika tarehe 29/6/2024.
Kuhusu changamoto zilizoelezwa awali na baadhi ya Wananchi wa Kabanga ambapo mradi huo unatekelezwa, DC Kahabi aliwapa nafasi Wananchi hao kuuliza maswali toka kwa Meneja wa TARURA na Wataalam wake na majibu mazuri na ya kuridhisha yalitolewa kwa Wananchi hao.
Aidha, Mhe DC Kahabi aliwaagiza TARURA kuongeza kasi ya Ujenzi huo na kuhakikisha wanakamilisha ndani ya muda uliopo kwenye Mkataba.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa