- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe. Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Ngara akifuatana na Ndg. Solomon Kimilike Mkurugenzi Mtendaji Ngara pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama wamefanya ziara ya ukaguzi ujenzi wa soko la Kahaza kata ya Rusumo ambapo bado Kazi inaenda Kwa kusuasua
"Kwa kuwa Kasi ya ujenzi Bado ni ndogo nitaongeza muda zaidi wakuwa nafuatilia Kila baada ya siku chache" amesema Mhe Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mhe Mkuu wa Wilaya amemshukuru Ndg Solomoni Kimilike DED Ngara Kwa ushikiano mkubwa anaoupata kutoka kwake "Mkurugenzi anahakikisha hakuna kinachokwama kilicho ndani ya uwezo wake na ni msikivu na mwepesi wakupokea maelekezo tuendelee hivihivi Ili tuendelee kuwa faida Kwa wananchi wa Ngara bega Kwa bega" amesema Mhe Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Wilaya Mhe Kanali Kahabi ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani anatoa fedha nyingi za Miradi ya Maendeleo Wilayani Ngara na wananchi waendelee kumuunga mkono Ili kazi iendelee.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa