- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col. Mathias Julius Kahabi amefanya ziara katika kijiji cha mkalinzi kata ya Muganza ambapo katika ziara hiyo ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Usalama Wilaya, Viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya wakiongozwa na Mkiti Mhe Vitalis Ndailagije, Mhe Diwani na viongozi wa Kata ya Muganza , Wataalam toka Halmashauri wakiongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg Enock Mponzi.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa kufuatilia tuhuma dhidi ya Viongozi wa Kijiji hicho hususan Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Bw Richard Mavogoro kutuhumiwa kugawa ardhi maeneo ya Tingatinga katika Kitongoji cha Musaza.
Mhe.Mkuu wa wilaya katika kikao alizungumza na Viongozi wa CCM ngazi ya Kata na Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na baadhi ya wananchi na kutoa maagizo mbalimbali ambapo ameagiza kusimamisha shughuli zote kwenye matingatinga hayo mpaka taratibu zitakapofuatwa, kushirikiana na wananchi pamoja na Halmashauri ya Kijiji wakati wa kugawa maeneo hayo, kuhakikisha ugawaji unafuata taratibu Kwa waombaji kutuma maombi Kwa kuandika barua.
Aidha Mhe kahabi amesisitiza Serikali ya Kijiji kutogawa maeneo ambayo yana migogoro na kuhakikisha uongozi wa Kata unashirikiana na Serikali ya Kijiji kutambua maeneo yaliyovamiwa.
Mwisho Mhe. Kahabi amewataka wananachi kujiandaa Kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua Viongozi bora watakaowaletea maendeleo na kupunguza migogoro ya jamii hususan ya ardhi ambapo jamii imekuwa ikikumbana na changamoto hiyo mara kwa mara.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa