- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tarehe 20/01/2024, Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara akifuatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Solomon Kimilike, Wataalam toka Halmashauri na Wasimamizi wa miradi ya LADP - 2, Viongozi wa Kijiji cha Rusumo pamoja na Mkandarasi wa mradi wa Soko la Kimkakati Rusumo walifika katika eneo la mradi na kukagua maendeleo ya Ujenzi huo ambapo Viongozi hao wameridhishwa na Ujenzi huo.
Ambao ulianza kwa kusua sua. Kwa sasa Ujenzi huo uko zaidi ya asilimia 18 na unatarajiwa kukamilika tarehe 31/03/2024 na utagharimu kiasi cha Shs bilioni 2.5.
Aidha, kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Ngara, Mkuu wa Wilaya Mhe. Col Kahabi kwa heshima na unyenyekevu mkubwa anaendelea kumpongeza na kumshukuru Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kufanikisha Miradi hii ya Kimkakati kutekelezwa Wilayani Ngara.
Mhe col Mathias J. Kahabi Mkuu wa Wilaya ya Ngara akiwa na viongozi Mbalimbali aliambatana nao katika Ukaguzi wa Ujenzi wa soko Mkakati la Kahaza kata ya Rusumo Wilayani Ngara.
Mafundi wakiwa kazini.
Ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa