- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Uongozi wa NELSAP ukiongozwa na Project Manager - Regional Rusumo Falls Hydro Electric Project Ndg. Alloyce Oduor akifuatana na Ndg Mansour Hamdun Rashid - Lead Environment and Social Safeguard Specialist walifika Ofisini kwa Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa Wilaya Ngara kwa ajli ya kutoa taarifa ya Maendeleo wa Ujenzi/Ukarabati wa nyumba zaidi ya 500 Waguswa wa milipuko wakati wa utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa maporomoko ya Rusumo.
Mradi unaotekelezwa kwa Ushirikiano wa Nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi. Mradi huo sasa umefikia zaidi ya asilimia 99 . Aidha, Viongozi hao pamoja na mambo mbalimbali waliyojadiliana katika Kikao hicho, wamekubaliana kufanya Mkutano mkubwa wa pamoja utakaoshirikisha Viongozi wa Wilaya, Uongozi wa NELSAP, Viongozi wa Kata na Serikali ya kijijni cha Rusumo pamoja na Wananchi wote wa Kijiji cha Rusumo.
kwa lengo la kutoa taarifa ya maendeleo ya Mradi huo na kusikiliza kero za wananchi hao na kuzitolea ufumbuzi.
Serikali ya Mhe Dr Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo kazini Wilayani Ngara na kazi iendelee.
Mhe Col.Mathias J. Kahabi akiwa na katibu Tawala Wilaya Bi Hatujuani A. Lukali, Afisa Tarafa Nyamiaga, Ndg Jawadu Yusuph, Mwakilishi wa Dso, pamoja na viongozi wa Nelsap.Ofisini kwake Mhe Mkuu wa wilaya.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa