- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya NGARA Mhe Col Mathias Julius Kahabi, amempongeza Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara - Afande William Solla na Kamati ya Usalama ya Wilaya kwa kuanzisha zoezi Maalum la Utoaji Elimu kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngara kutokana na matukio ya baadhi ya Wananchi kujitoa uhai kwasababu mbalimbali ikiwemo wivu wa mapenzi, migogoro ya kifamilia nk.
Mhe DC Kahabi amefurahishwa na kitendo cha OCD Solla kuchukua haraka azimio la Kamati ya Usalama la hivi karibuni kutaka hatua za haraka kuchukuliwa kuelemisha jamii yetu kufuatia taarifa mbalimbali za Matukio ya namna hiyo kuendelea kiripotiwa Wilayani Ngara.
OCD Kamanda Solla na Askari wake amesema zoezi hili litakuwa endelevu na litafanyika katika Kata zote 22 za Wilaya ya Ngara na baadhi ya Vijijini ambapo amewataka Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kukomesha matukio haya na kuendelea kufanya Wilaya ya Ngara kuwa kitovu cha amani na Utulivu ndani ya Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla.
Ngara Kazi inaendelea..
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa