- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA UPDATE
Leo Tarehe 22/10/ 2024, Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ameshuhudia tukio la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Ndg Solomon Kimilike na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Wilbard Bambara, Wakisaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa mwaka 2024/2025 kati ya Halmashauri na Kampuni ya Tembo Nickel.
Kwa mkataba huu Tembo Nickel watatekeleza miradi ya Elimu na afya.
Aidha, Mwakilishi wa Uongozi wa Tembo Nickel Ndg Moses Rusasa alitoa maelezo juu ya maendeleo ya Mradi ambao kwa sasa umefikia hatua nzuri kwenye ulipaji fidia kwa Waguswa wa Mradi huo.
Mkiti wa Halshauri ya wilaya Mhe Wilbard Bambara na Mkuurugenzi Mtendaji wilaya Ndg Solomon Kimilike pamoja na viongozi Tembo Nickel wakiwa na Mhe Col Mathias J kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara.
Picha ya pamoja baada ya kumaliza kusaini Mkataba ofisi kwa Mhe mkuu wa wilaya.
Ngara Kazi inaendelea.
www.ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa