- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ngara.
Mhe Col Mathias Julius Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara, amefanya Kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi cha Wilaya na Wajumbe wa Kikao hicho .
ambapo wamejadili na kuweka Maazimio mbalimbali kuhusiana na Suala zima la Wafanyabiashara kuhusu wajibu wao wa kulipa Kodi kwa maendeleo na manufaa ya Nchi.
Aidha, Mkuu wa wilaya col.Kahabi amewasihi Wafanyabiashara hao kujiepusha na tabia za ukwepaji wa kulipa Kodi ya Serikali na kuwaomba kulipa kwa wakati na bila shuruti kwa Mujibu wa Sheria za Kikodi zilizopo.
Kwa upande wa biashara haramu ya magendo Mhe. Col Mathias Julius Kahabi amesema ni maarufuku kwa mfanyabiashara yeyote kufanya biashara ya magendo toka nchi jirani zipakanazo wilaya ya Ngara yaani Burundi na Rwanda. Bidhaa na biashara halali zote lazima zipite katika mipaka yetu rasmi ya Murusagamba, Kabanga na Rusumo ili Mhusika aweze kulipa Kodi stahiki tofauti na hapo Mkuu wa wilaya Kahabi amesema njia zisizokuwa rasmi haziruhusiwi kupitisha Biashara na bidhaa zozote kwa sababu zinapita kwa njia ya magendo na hivyo kuikosesha Serikali mapato yake halali.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa