- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Mhe Col.Mathias J.kahabi amefanya Kikao na viongozi wa NELSAP, viongozi Toka Kijiji Cha Rusumo, Afisa Tarafa na Kamati ya BMC.
Viongozi wengine walishiriki Kikao hicho ni Katibu Tawala Wilaya , DSO, PCCB,Mhandisi Mshauri, Afisa ardhi Wilaya.pia Wakandarasi wanaojenga na kukarabati Nyumba zilizoathiriwa na Blasting wakati wa utekelezaji wa Mradi wa umeme Rusumo.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Radio Kwizera uliopo Ngara Mjini.
Lengo la kikao Ikiwa ni kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika kazi ya ujenzi na Ukarabati wa nyumba zilizoathiriwa wakati wa Mradi wa umeme Rusumo Wilayani Ngara.
Ukarabati na ujenzi utahusisha majengo 540 na utagharimu zaidi ya Tsh Bilion 7.5
Aidha imeelezwa kuwa tayari Malipo mbalimbali yameanza kutolewa Kwa wananchi waliotakiwa kupisha Ukarabati.
Baada ya majadiliano Mhe Col Mathias Kahabi Mkuu wa wilaya ya Ngara ameagiza yafuatayo.
1. Ushirikishwaji wa pamoja Kila linalofanyika
2. kamati ya BMC wapewe ushirikiano
3. Changamoto zote zichukuluwe na kutatuliwa
4. wanufaika waoneshwe michoro ya majengo Yao kuwa wazi.
5. kasi ya ujenzi iongezeke Ili kazi ikamilike Kwa wakati.
6. Wakandarasi wawepo eneo la ujenzi (site) muda wote
7. Imeundwa kamati ya ufuatiliaji wa waathirika ambao nyumba zao hazikufanyiwa Tathmini baada ya kamati kuwasilisha taarifa Kwa Mhe Mkuu wa wilaya Kwa kushirikiana na NELSAP Atafanya Mkutano na Wananchi wote wa Kijiji Cha Rusumo Ili Kutoa Mrejesho wa Maendeleo ya kazi na jinsi changamoto ilivyotatuliwa.
8. Viongozi wa Serikali ,Chama wanasimama upande wa wananchi Ili kupata haki zao.
Mkuu wa wilaya Mhe Col Mathias J Kahabi akiwa na katibu Tawala Bi Hatujuani A.Lukali wakiwa kwenye Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Radio Kwizera.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Radio kwizera iliopo Ngara Mjini.
Viongozi wakiendelea na Kikao.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa