- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za uwekezaji
- Huduma zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
NGARA LEO 11/3/2024.
Mhe Col Mathias Julius Kahabi DC Ngara, ametoa pongezi nyingi kwa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa kutembelea na kukagua Ujenzi wa Jengo la Halmashauri Head Quarters (HQ) Wilaya ya Ngara unaotekelezwa na Kampuni ya Home Africa co.Ltd. Ujenzi huo hadi umefikia asimilia 55 na unatarajiwa kukamilika mwezi Jun 2024 na kugharimu kiasi cha Shs bilioni 3.5.
Ziara hiyo iliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mhe Bulindori ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe Wilbard Bambara.
Aidha, Mhe DC Kahabi anatoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Solomon Kimilike kwa usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa mradi huo.
Pia kwa namna ya kipekee kabisa Mhe Col Mathias Kahabi DC Ngara anaendelea kutoa pongezi na shukrani za dhati kwa Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia kutoa kiasi cha Shs bilioni 3.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi huu mkubwa Wilayani Ngara.
Kazi iendelee.
ngaradc.go.tz
Ngara District Council
Anuani ya Posta: P.O.Box 30, Ngara
Simu ya mezani: 0282226016
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@ngaradc.go.tz
Hakimilki ©2017 Halmashauri ya wilaya ya Ngara. Haki zote zimehifadhiwa